| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Wabunge Ufaransa kujadili mswada wa kurudisha kazi za sanaa zilizoibiwa Afrika wakati wa ukoloni
Bunge la Ufaransa linahitaji kila kitu kilichopo katika makumbusho ya taifa kupigiwa kura kimoja kimoja.
Wabunge Ufaransa kujadili mswada wa kurudisha kazi za sanaa zilizoibiwa Afrika wakati wa ukoloni
Mataifa ya kikoloni Ulaya yameanza pole pole kurudisha baadhi ya kazi za sanaa zilizochukuliwa wakati wa ukoloni. / Reuters / Reuters
13 Aprili 2026

Wabunge wa Ufaransa Jumatatu watajadili mswada wa kurahisha kurudisha kazi za sanaa zilizoibiwa wakati wa ukoloni katika nchi zao za asili.

Ufaransa bado ina maelfu ya kazi za sanaa na vito vyengine vyenye thamani ambavyo viliibiwa wakati wa ukoloni.

Rasimu hiyo ya mswada ya kuvirudisha ilipigiwa kura ya wingi katika bunge la juu mwezi Januari, na sasa hivi inasubiri kuungwa mkono katika bunge la taifa kabla ya kuwa sheria.

Rais Emmanuel Macron ametoa ahadi ya kurudisha kazi hizo za kitamaduni, tofauti na watangulizi wake katika kukiri uovu uliofanywa na Ufaransa katika mataifa ya Afrika.

Akizungumza katika ziara yake mjini Ouagadougou nchini Burkina Faso, punde tu baada ya kuingia madarakani mwaka 2017, Macron aliapa kwamba Ufaransa katu haitaingilia tena makoloni yake na kuahidi kuwezesha urudishaji wa hazina za Afrika ndani ya miaka mitano.

Mswada huo unalenga zaidi mali zilizopatikana kati ya miaka 1815 na 1972.