Marekani inafikiria upya kufanya mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran baada ya mazungumzo ya amani nchini Pakistan kushindikana, limeripoti jarida la The Wall Street Journal.
Makamu wa Rais JD Vance na ujumbe wake ulioongoza mazungumzo mjini Islamabad, lakini majadiliano yaliisha bila kufikia makubaliano.
Rais Donald Trump amesema washauri wake wameangalia uwezekano wa kuanza kwa mashambulizi katika baadhi ya maeneo nchini Iran pamoja na Marekani kuzuia meli kuingia na kutoka kwa meli katika Mlango Bahari wa Hormuz, kama njia moja wapo ya kukabiliana na mkwamo uliopo, limeripoti jarida hilo siku ya Jumapili.
Akizungumza kutoka Florida, Trump ameiambia Fox News kwamba vinu vya umeme vya Iran pamoja na miundombinu ya maji vinaweza kushambuliwa iwapo hali itazidi kuwa tete.
"Sipendi kufanya hivi, lakini ni maji yao, vituo vyao vya kusafisha maji, vinu vyao vya kufua umeme, ambavyo ni rahisi sana kushambuliwa," amesema, akiweka wazi kwamba yote hayo yapo mezani.
Mkakati wa kufunga Hormuz
Msemaji wa ikulu ya White House, Olivia Wales amesema Rais "kwa busara ameweka mipango yote mezani," huku akithibitisha uzuiaji wa Mlango Bahari wa Hormuz unaofanywa na vikosi vya majini una lengo la kusitisha "toza ya Iran."
Marekani inataka Iran kusitisha mpango wake wa kurutubisha urania, kuharibu mitambo, na kukubali mpango mpana wa ulinzi.
Uzuiaji wa Hormuzi una lengo la kuzuia mapato ya mafuta ya Iran, ambayo yanaendesha takriban nusu ya bajeti ya serikali.
Hata hivyo, mpango huo una hatari, kwa sababu meli za vikosi vya majini za Marekani zilizopo karibu na Mlango Bahari wa Hormuz zinakabiliwa na tishio la kushambuliwa.













