| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Kampuni ya BP yashtakiwa Kenya kufuatia madai ya uchafuzi mazingira kutokana na uchimbaji mafuta
Mahakama Kuu nchini Kenya imeamua Alhamisi kuwa kesi dhidi ya Kampuni ya kimataifa ya mafuta na gesi BP, inayodai uchafuzi wa mazingira wa miongo kadhaa uliosababisha kuingia kwenye maji ya kunywa kaskazini mwa Kenya, inaweza kuendelea.
Kampuni ya BP yashtakiwa Kenya kufuatia madai ya uchafuzi mazingira kutokana na uchimbaji mafuta
BP imeshtakiwa Kenya kwa madai ya kuwepo kwa uchafu hatari kwenye visima vya mafuta kaskazini mwa Kenya. / Reuters
16 Aprili 2026

Mahakama Kuu nchini Kenya imeamua Alhamisi kuwa kesi dhidi ya Kampuni ya kimataifa ya mafuta na gesi BP, inayodai uchafuzi wa mazingira wa miongo kadhaa uliosababisha kuingia kwenye maji ya kunywa kaskazini mwa Kenya, inaweza kuendelea.

Kesi hiyo, iliyowasilisha na walalamikaji 299 mwezi Februari katika Mahakama ya Ardhi na Mazingira mjini Isiolo, inadai kuwa BP ilisababisha uchafuzi hatari wa mazingira kwa kutupa uchafu kwa njia isiyo sahihi uliotokana na shughuli zao za uchimbaji mafuta katika baadhi ya sehemu za kaskazini mwa Kenya.

Inadai uchafu huo, uliingia kwenye maji ardhini na kuwafanya mamia ya wakazi na mifugo kuwa wagonjwa na wengine kufariki.

“Wakati wa uchimbaji mafuta, uchafu wenye sumu ulitupwa kwa njia isiyo sahihi na kuingia katika mazingira,” madai hayo yalisema.

Vifo vilivyotokana na saratani

Uchimbaji huo wa mafuta ulifanyika katika miaka ya themanini na kampuni ya Amoco, ambayo baadaye ilinunuliwa na BP 1998. Katika kipindi hicho, Amoco ilichimba visima kadhaa karibu na Kargi na Kalacha katika Jangwa la Chalbi kaskazini mwa Kenya.

Pia inadai kuwa wakazi zaidi ya 500 waliokuwa wanaishi karibu na maeneo ya uchimbaji mafuta walifariki kutokana na maradhi yanayohusiana na saratani na magonjwa mengine kwa kunywa maji ambayo yalikuwa na sumu.

Kesi hiyo inatarajiwa kuanza tena mwezi Mei. BP bado haijatoa taarifa yoyote kwa umma kujibu madai hayo na haikujibu barua pepe waliotumiwa na shirika la Associated Press kutaka wazungumzie suala hilo.

CHANZO:TRT Afrika Swahili