Watu wa kabila la WaIgbo wamepigwa marufuku kusimika ‘’wafalme’’ nje ya Nigeria.
Hili linafuata utata wa hivi karibuni ambapo ‘’Mfalme wa Igbo’’ alisimikwa nchini Afrika Kusini, jambo lililozua hasira miongoni mwa raia wa Afrika Kusini.
Sasa baraza la kijamii na kitamaduni la WaIgbo kote duniani, Ohaneze Ndigbo, limepiga marufuku kwa hafla kama hizo kufanyika nje ya nchi. Serikali ya Nigeria imeunga mkono uamuzi huo.
Waziri wa Nchi wa Mambo ya Nje wa Nigeria Bianca Odumegwu-Ojukwu, ambaye alihudhuria mkutano wa bodi hiyo ya juu ya maamuzi Ohaneze ambapo uamuzi huo ulitangaza Aprili 9 mji wa Enugu, anasema ‘’wasiwasi wa kusimika 'wafalme' wa Igbi nje ya nchi’’ umeharibu sifa ya Nigeria na kuathiri uhusiano wa kidiplomasia.
Bianca Odumegwu-Ojukwu, ambaye ni wa jamii wa Igbo, anasema kusimika viongzoi wa wa kijadi nje ya nchi kunachukuliwa kama ‘’kukejeli watu wanaoishi katika nchi hiyo’’.
‘Disrespectful’ act
Aliongeza ‘’kujikweza’’ na ‘’kuonesha utajiri kwa Wanigeria’’ wakati wa hafla hizi ilhali wakati mwingine raia wa nchi hizo wanakabiliwa na changamoto za kiuchumi ‘’ni dharau ya wazi.’’
Waziri huyo alisema mabalozi ya Nigeria nje na nchi wenyeji watafahamishwa kuhusu marufuku hiyo.
Alieleza kuwa watu wa jamii ya Igbo waliopo nje ya nchi wana haki ya kutangaza utamaduni wao, lakini wanatakiwa kuzingatia wakazi wa nchi wenyeji.
Katika taarifa, Bianca Odumegwu-Ojukwu amesema viongozi wa Igbo nje ya nchi wanaweza kuitwa ‘’Onyendu’’ ambayo inamaanisha kiongozi badala ya ‘’Igwe’’ au ‘’Eze’’ kumaanisha mfalme.
Marufuku hii inakuja karibu mwezi mmoja baada ya mwanamume raia wa Nigerian, Chifu Solomon Ogbonna Eziko, kusimikwa kuwa "Igwe Ndigbo Na eneo la East London", tafsiri yake ikiwa ni ‘’mfalme wa Igbo wa East London,’’ mji ulioko Mkoa wa Eastern Cape wa Afrika Kusini.
Hili lilisababisha hasira kutoka kwa wenyeji na mamlaka nchini Afrika Kusini, walioona kama "kukosa heshima" kwa sheria za Afrika Kusini na tamaduni.
Baadaye Nigeria iliomba radhi, huku wanadiplomasia wakiingilia kati kutatua suala hilo.















