| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Raia wa China ahukumiwa jela kwa kusafrisha mchwa kutoka Kenya kinyume cha sheria
Raia wa China aliyekamatwa akijaribu kusafirisha mchwa kutoka Kenya kinyume cha sheria amehukumiwa kulipa faini na kifungo gerezani.
Raia wa China ahukumiwa jela kwa kusafrisha mchwa kutoka Kenya kinyume cha sheria
Zhang Kequn, raia wa China, amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kusafirisha mchwa kinyume cha sheria. / / Reuters
tokea masaa 3

Zhang Kequn alikamatwa mwezi Machi katika uwanja wa ndege wa JKIA akiwa na zaidi ya mchwa 2,200.

Mahakama ya Kenya siku ya Jumatano, Aprili 15, iliamuru raia huyo wa China aliyepatikana akijaribu kusafirisha mchwa hai nje ya nchi kinyume cha sheria kulipa faini ya shilingi milioni 1 (dola 7,746) na kutumikia kifungo cha miezi 12 gerezani.

Jaji katika kesi hiyo alisema adhabu kali ilihitajika ili iwe fundisho kwa wengine, kufuatia kuongezeka kwa visa kama hivyo nchini Kenya.

Wadudu hao mara nyingi husafirishwa China, Marekani na Ulaya, ambako hufugwa majumbani na thamani ya mdudu mmoja inakaribia dola 100 za Marekani.

Usafirishaji wa mchwa ulivuta hisia kubwa za vyombo vya habari mwaka jana baada ya vijana wawili kutoka Ubelgiji kukamatwa wakiwa na karibu mchwa 5,000, na kutozwa faini ya takribani dola 7,700.

CHANZO:AFP