Mkutano wa 5 wa Jukwaa la Kidiplomasia la Antalya umeanza siku ya Ijumaa nchini Uturuki, ukiwaleta pamoja viongozi mbalimbali duniani kuzungumzia hali ya sasa ulimwenguni.
Likiwa limeandaliwa na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki, jukwaa hilo la siku tatu linafanyika katika mji wa kitalii wa Antalya, chini ya kauli mbiu Maandalizi ya Kesho, Kutatua Wasiwasi.
Zaidi ya mataifa 150 yanahudhuria jukwaa hilo, wakiwemo zaidi ya wakuu wa nchi zaidi 20.
Jukwaa hilo, pia linawaleta pamoja zaidi ya mawaziri 50, na wawakilishi kutoka mashirika 75 ya kimataifa.
Kwa ujumla, zaidi ya washiriki 5,000 wanatarajiwa kuhudhuria tukio hilo, huku nusu yao wakitokea Afrika na Ulaya.
Mawaziri wa mambo ya nje kutoka Afrika, Ulaya na Asia wanatarajiwa kuhudhuria jukwaa hilo.
Kutakuwa na zaidi ya majopo 40 wakati wa jukwaa hilo, ambao yatahusisha mijadala kuhusu uongozi, uchumi, mazingira, siasa na teknolojia.
Mijadala hiyo itarushwa moja kwa moja kupitia tovuti na mitandao ya kijamii, pamoja na choombo cha habari cha TRT.
Wakati wa jukwaa hilo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan anatarajiwa kuhudhuria vikao tofauti, ikiwemo cha Gaza.


























