Mkuu wa Mawasiliano wa Uturuki Burhanettin Duran ameadhimisha miaka 106, toka kuanzishwa kwa shirika la habari la Anadolu.
Akizungumza jijini Ankara, Duran alisema shirika hilo lililoanzishwa mwaka 1920, kuihabarisha dunia kuhusu yanayoendelea Uturuki, limekuwa chombo muhimu cha kuhabarisha ulimwengu, chini ya uongozi wa Rais Recep Tayyip Erdogan.
“Inatia faraja sana kuona namna shirika la Anadolu lilivyokuwa,” alisema Duran.
Mkuu huyo wa Mawasiliano wa Uturuki amesema kuwa shirika hilo linalenga kuwa kati ya mashirika makubwa duniani, akisisitiza namna lilivyojiimarisha kiteknolojia.
Kulingana na Duran, kwa sasa Anadolu limekuwa shirika si tu, lenye kuhabarisha mambo ya ulimwenguni, bali ni shirika lenye kuchagiza haki, usawa na tunu zingine duniani.
Alitumia fursa hiyo kuwashukuru wafanyakazi wa shirika hilo kwa michango yao ya hali na mali.
Shirika la Anadolu lilianzishwa Aprili 6, 1920 chini maelekezo ya Mustafa Kemal Ataturk, wakati wa vita vya kupigania uhuru, kwa nia ya kuhabarisha umma kuhusu yaliyokuwa yanajiri kwa wakati huo.

















