Uturuki inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano muhimu wa diplomasia wa kikanda mjini Antalya, ukiwaleta pamoja Uturuki, Misri, Pakistan na Saudi Arabia kujadili mipango ya kuratibu na kukabiliana na mizozo katika kanda, ikiwemo vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.
Utakuwa mkutano wa tatu wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Misri, Pakistan na Saudi Arabia, mwenyeji akiwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan pembeni mwa Jukwaa la Diplomasia la Antalya 2026 siku ya Ijumaa, kulingana na vyanzo vya kidiplomasia.
Kujumuika huku kunakuja huku diplomasia ya kikanda ikiendelea kushika kasi, na nchi zinazoshiriki zikitaka mtazamo wa pamoja katika masuala kadhaa ya kukabiliana na changamoto za usalama na kisiasa.
Mazungumzo hayo yanatarajiwa kuangazia namna ya kukabiliana na matatizo ya kikanda kama kanda, vyanzo vimesema huku msisitizo ukiwa kwa hali ya taharuki inayohusisha Marekani, Israel na Iran, chini ya mfumo wa kanda kuhusika na majadiliano.
Mkutano huo unafuata misururu ya mikutano ya ngazi za juu ya kidiplomasia miongoni mwa nchi hizo.
Machi 18 mjini Riyadh, mawaziri wa mambo ya nje walikuwa na mkutano kujadili yanayojiri katika kanda na mabadiliko ya siasa duniani, uliojumuisha Uturuki, Azerbaijan, Qatar, Bahrain, Misri, Jordan, Kuwait, Lebanon, Pakistan, Saudi Arabia, Syria na UAE.
Kufuatia kikao hicho, Uturuki, Saudi Arabia, Pakistan na Misri wakawa na mkutano mwingine pembeni kwa mkutano mkuu.
Mkutano huo ulikuwa sehemu ya juhudi zaidi za kuimarisha mifumo ya kushauriana kote katika kanda.
Mfumo huu wa pembe nne badaaye uliendelea tena mjini Islamabad Machi 29, ambapo mwanadilplomasia mwandamizi wa Uturuki Hakan Fidan na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo tatu walihudhuria kikao hicho cha pili.
Mkutano wa mwisho wa mfumo huo huo ulifuata katika ngazi ya manaibu uliofanyika mjini Islamabad Aprili 14.
















