Maonesho ya Kimataifa ya Uturuki ya SAHA 2026 kuhusu Ulinzi na Anga yameanza katika ukumbi wa Expo wa Istanbul siku ya Jumanne, huku makampuni 1,700, ikiwemo 263 ya kimataifa na zaidi ya wataalamu zaidi ya 30,000 katika sekta hiyo kutoka nchi zaidi ya 120 wakihudhuria.
Maonesho hayo yameandaliwa na SAHA Istanbul, muungano mkubwa wa Uturuki na Ulaya katika sekta ya ulinzi, na anga.
Maonesho hayo yanafanyika katika ukumbi wa Istanbul Expo hadi Mei 9.
Yakiwa katika eneo la ndani na nje lenye ukubwa wa mita mraba 400,000 (futi mraba milioni 4.3), SAHA 2026 imetenga mita mraba 20,000 (karibu futi mraba 215,300) kwa ajili ya eneo la nje, kufanya kuwa maonesho makubwa zaidi tangu kuanza kwake.
Makampuni zaidi ya 1,700, ikiwemo mashirikia 263 ya kimataifa, na wataalamu zaidi ya 30,000 katika sekta hiyo kutoka zaidi ya nchi 120 yanahudhuria maonesho hayo.
Kutakuwa na vifaa vipya 203 ambavyo vitaoneshwa, na hafla 164 za utiaji saini zitafanyika katika SAHA 2026. Hafla hiyo inalenga kuongeza mikataba ya mauzo ya nje kutoka Dola bilioni $6.2 ya SAHA 2024 hadi kiwango kisichopungua Dola bilioni $8 mwaka huu.
Kuna washiriki kutoka Ulaya, Marekani na Canada, huku makampuni mengi, wawakilishi wa mashirika, maafisa wa serikali, wajumbe wa biashara na wageni kutoka mabara manne wakihudhuria hafla hiyo.
Vifaa kadhaa vya teknolojia ya juu na vyenye ubora zaidi vitakuwepo kwa baadhi ya watu duniani kuviona kwa mara ya kwanza katika SAHA 2026. Meli za jeshi la wanamaji zilizotengenezwa Uturuki pia zitaoneshwa katika eneo la Atakoy Marina kama sehemu ya maonesho hayo.
Makampuni ya ulinzi ya Uturuki yazindua teknolojia mpya
Kutakuwa na teknolojia mbalimbali ambazo zitazinduliwa kwa mara ya kwanza katika maonesho ya SAHA 2026.
Kampuni kubwa ya kutengeneza droni ya Uturuki Baykar itaonesha MIZRAK, iliotengenezwa nchini na yenye uwezo ya kwenda umbali wa zaidi ya kilomita 1,000 na kutumia akili unde (AI).
Pia Baykar itaonesha K2 Kamikaze UAV na Sivrisinek kwa mara ya kwanza kwenye maonesho ya SAHA 2026.
Kampuni nyingine kubwa ya ulinzi ya Uturuki, Aselsan, itaonesha vifaa vyake vipya vitano na vifaa sita vya sasa vilivyoimarishwa, kuleta pamoja teknolojia za taifa na mifumo ya ulinzi ya dunia.
Mfumo wa Silaha za Nishati, uliotengenezwa kwa ushirikiano kati ya Roketsan na FNSS na unaojulikana maarufu kama “silaha ya mwanga,” pia utakuwepo kwenye maonesho ya SAHA 2026 ukiwa na uwezo zaidi.
Kampuni ya vifaa vya ulinzi ya Uturuki Roketsan itaonesha vifaa vyake vipya na vyenye uwezo kwenye maonesho hayo kwa mara ya kwanza, huku STM ikionesha mifumo ya anga na kwenye maji iliotengenezwa kwa ajili ya uwezo wa vita kisasa kwa mara ya kwanza.
Maonesho hayo yatakuwa na ujumbe rasmi zaidi ya 140, wakiwa na wajumbe rasmi zaidi ya 800, na wawakilishi zaidi ya 200 wa masuala ya biashara.
SAHA 2026 itafunguliwa kwa ajili ya umma Mei 9 kama sehemu ya kuruhusu kila mtu kwenye maonesho hayo.




















