Ni Maporomoko ya Maji ya Murchison, ambayo yapo kaskazini-magharibi mwa Uganda kwenye Mto Nile.
Hapa takriban lita 300,000 za maji zinapenya kwa sekunde kwenye njia nyembamba yenye upana wa kati ya mita 7 hadi 8.
Maji haya yanashuka kwa kasi kubwa hivyo huzalisha mngurumo wa radi, mwendo wa kasi, na upinde wa mvua au rainbow wa kudumu, na kusababisha mtetemeko katika eneo lililozunguka.
Kupitia mtiririko huu wa maji kuelekea Ziwa Albertm, ni moja wapo ya sehemu ya kuvutia ya kuangalia wanyamapori nchini Uganda.
Ni mandhari ya kipekee iliyojaa wanyama pori kama vile tembo, twiga, na nyati kwenye kingo za mito, huku viboko, mamba na ndege wa majini wakiwa wakazi wa kudumu wa eneo hilo.
Maporomoko ya Murchison, pia yanajulikana kama Maporomoko ya Kabalega, yaliyopewa jina la Omukama au Mfalme wa watu wa Bunyoro wa Uganda.
Mwaka 1972, aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Idi Amin aliyabadilisha jina na kuyaita Maporomoko ya Kabalega, ili kumuenzi Mfalme Kabalega ambaye aliongoza vita vya miaka mitano dhidi ya upanuzi wa Waingereza (1894–1899) na baadaye kuhamishwa hadi Ushelisheli.
Maporomoko hayo yalizingatiwa kuwa eneo takatifu, huku jamii za wenyeji zikitumia mkondo wa maji kutabiri mifumo ya hali ya hewa na kutoa kafara za kitamaduni.
Kivutio maarufu zaidi cha kiutalii kwenye maporomoko ya maji ni safari ya hadi saa 3 kuelekea eneo hilo.
Maporomoko hayo ni sehemu ya Mbuga ya Kitaifa ya Murchison Falls kivutio kikubwa na cha kihistoria cha watalii kwa Uganda.
Hifadhi hiyo ina aina 76 za mamalia, pamoja na wale wanyama wakubwa watano yani simba, chui, tembo, na nyati. Pia kuna idadi kubwa ya twiga wa Rothschild duniani.
Ikiwa na zaidi ya spishi 450 za ndege, mbuga hii ni mahali pa juu zaidi kwa ndege, haswa kwa kuona korongo adimu katika Delta ya Nile-Ziwa Albert.
Kusini mwa msitu huu ni mahali pazuri kwa ufuatiliaji wa maisha ya sokwe.
Uzuri huu wote wa asili umevikwa taji na Maporomoko ya Murchison.
Kwa hivyo, unapokuwa Uganda, ni muhimu kushuhudia maporomoko ya maji ambayo ni moja ya vivutio muhimu nchini humo.













