| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Fidan afanya mazungumzo na Balozi wa Marekani, Katibu Mkuu wa muungano wa OTS jijini Ankara
Hakan Fidan akutana na Tom Barrack, Darrell Issa, na Kubanychbek Omuraliev ili kujadili uhusiano wa pandi mbili na maandalizi ya mkutano wa kilele wa OTS unaotarajiwa kufanyika.
Fidan afanya mazungumzo na Balozi wa Marekani, Katibu Mkuu wa muungano wa OTS jijini Ankara
Fidan amekutana an mjumbe wa Marekani Tom Barrack na mbunge wa Marekani Darrell Issa jjini Ankara, tarehe 8 Septemba 2026. /

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, amekutana na Balozi wa Marekani nchini Uturuki, Tom Barrack, mbunge wa Baraza la Wawakilishi la Marekani anayemaliza muda wake, Darrell Issa, na Katibu Mkuu wa Muungano wa Mataifa yanayozungumza Kituruki (OTS), Kubanychbek Omuraliev, katika mji mkuu wa Ankara siku ya Jumanne.

Wizara ya mambo ya nje iliweka picha ya mkutano uliofanyika Ankara, lakini hakuna taarifa zaidi zilizopatikana mara moja.

Issa, ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Mahusiano ya Kigeni ya Baraza la Wawakilishi la Marekani, hatagombea tena katika uchaguzi wa wabunge wa Marekani utakaofanyika Novemba mwaka huu. Muda wake wa kuhudumu unatarajiwa kumalizika Januari mwakani, wakati mrithi wake atakapoapishwa na kuanza rasmi kazi katika Bunge jipya la Marekani.

Katika mkutano wake na Omuraliev, Fidan amejadili maandalizi ya Mkutano wa 13 wa Muungano wa Mataifa yanayozunumza Kituruki (OTS), ambao Uturuki itauandaa jijini Ankara tarehe 29 na 30 Oktoba, kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki.

CHANZO:AA