| Swahili
MICHEZO
1 dk kusoma
Mo Salah hatacheza mechi ya kufuzu AFCON dhidi ya Sudan Kusini kutokana na nyasi bandia za Uwanjani
Mohamed Salah hatasafiri na kikosi cha Misri kwenda Sudan Kusini kwa ajili ya mchezo wao wa pili wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika, kwa sababu mchezo huo utachezwa kwenye uwanja wenye nyasi bandia; hayo yamesemwa na Shirikisho la Soka la Misri
Mo Salah hatacheza mechi ya kufuzu AFCON dhidi ya Sudan Kusini kutokana na nyasi bandia za Uwanjani
Mohamed Salah wa Misri atakosa mechi ya kufuzu AFCON dhidi ya Sudan Kusini mnamo tarehe 29 Septemba 2026. / reuters

Mohamed Salah hatasafiri na kikosi cha Misri kwenda Sudan Kusini kwa ajili ya mchezo wao wa pili wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa sababu mechi hiyo itachezwa kwenye uwanja wenye nyasi bandia, Shirikisho la Soka la Misri (EFA) lilisema Jumamosi.

Misri ilitoka sare tasa na Angola katika Uwanja wa Kimataifa wa Cairo siku ya Ijumaa kwenye mchezo wao wa kwanza wa kufuzu.

Salah, ambaye hivi karibuni alijiunga na klabu ya Trabzonspor ya Uturuki akitokea Liverpool, alianza katika mchezo dhidi ya Angola lakini hakumaliza mechi hiyo baada ya kocha Hossam Hassan kumtoa uwanjani katikati ya kipindi cha pili.

"Benchi la ufundi la timu ya taifa ya Misri, likiongozwa na Hossam Hassan, limeamua kumpumzisha Mohamed Salah kwa ajili ya mchezo dhidi ya Sudan Kusini uliopangwa kufanyika Septemba 29 kutokana na aina ya uwanja utakaotumika," EFA ilisema kwenye mitandao ya kijamii.

Mechi itachezwa Juba

"Kulikuwa na makubaliano kati ya benchi la ufundi la timu ya taifa na Mohamed Salah kabla ya mchezo dhidi ya Angola kwamba hatacheza dhidi ya Sudan Kusini, na benchi la ufundi lilipendelea utaratibu huu ili kumlinda mchezaji huyo," EFA iliongeza.

Mechi kati ya Sudan Kusini na Misri itachezwa katika Uwanja wa Juba, ambao una nyasi bandia.

CHANZO:reuters