| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Vyama vya upinzani Burundi kumuunga mkono Ndayishimiye
Aprili mwaka jana, chama tawala cha nchini humo, CNDD-FDD, kilipitisha jina la Ndayishimiye kwa ajili ya uchaguzi huo wa mwakani.
Vyama vya upinzani Burundi kumuunga mkono Ndayishimiye
Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi.

Vyama 11 vya upinzani nchini Burundi, vimetangaza rasmi kumuunga mkono Rais Evariste Ndayishimiye katika uchaguzi mkuu wa urais uliopangwa kufanyika Mei 3, 2027.

Uamuzi huo ulitangazwa kupitia taarifa ya pamoja baada ya mkutano wa vyama hivyo uliofanyika jijini Bujumbura mnamo Novemba 10, 2026.

Vyama hivyo vimekubaliana kuunganisha nguvu na kufanya kampeni ya pamoja badala ya kusimamisha wagombea wao wenyewe.

Aprili mwaka jana, chama tawala cha nchini humo, CNDD-FDD, kilipitisha jina la Ndayishimiye kwa ajili ya uchaguzi huo wa mwakani.

CHANZO:TRT Afrika Swahili