Wake wa Marais wa Afrika: Rachel Chebet Ruto wa Kenya
Rachel Chebet Ruto lizaliwa Novemba 1969/ Picha: @MamaRachelRuto / Public domain
Wake wa Marais wa Afrika: Rachel Chebet Ruto wa Kenya
Rachel na William Ruto walifunga ndoa mwaka wa 1991, na wamebarikiwa watoto saba, mmoja wa kuasili.

Rachel Chebet Ruto ni mke wa Rais wa sasa wa Kenya, William Ruto. Alizaliwa Novemba 1969.

Alisomea Shahada ya Kwanza ya Elimu na kufanikiwa kupata Shahada ya Uzamili ya Sanaa mwaka wa 2011 katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki.

Ingawa alisomea Elimu, hakupata nafasi ya kufundisha kwa muda mrefu kwani alistaafu kwa hiari yake na kujitosa katika ujasiriamali katika biashara ya utalii na usafiri.

Rachel na William Ruto walifunga ndoa mwaka wa 1991.

Mwaka 2009, alianzisha Shirika la ‘Joyful Women,’ mpango unaolenga kuwawezesha kifedha wanawake wa vijijini.

Alihudumu kama mke wa Naibu Rais kati ya mwaka 2013 na 2022 wakati mume wake alipokuwa Naibu wa Rais wa Kenya.

Amepokea tuzo mbalimbali kutokana na mchango wake kwa jamii katika uhifadhi wa mazingira na pia ukuzaji wa ustawi wa watu.

Miongoni mwa tuzo hizo, ni pamoja na tuzo ya heshima ya pili ya juu ya kiraia nchini Kenya; Tuzo ya Kuwainua Wanawake kutoka Chuo Kikuu cha Binary nchini Malaysia; na Tuzo ya Kibinadamu ya KISS ya 2023 kutoka India kwa ajili ya kutambua mchango wake wa kufanya mabadiliko kwa wanawake.

Mwaka 2021 Rachel Ruto aliteuliwa pia na Tume ya Umoja wa Afrika na Jukwaa la Kiuchumi Duniani kama mmoja wa Mabingwa wa AU katika Uwezeshaji wa Wanawake Kiuchumi na Ushirikishwaji wa Kifedha.

Katika ngazi ya bara, Rachel Ruto anahudumu kama mjumbe wa Kamati ya Uongozi wa Shirika la Wanawake wa Marais wa Afrika kwa Maendeleo (OAFLAD), ambapo anachangia kubuni mikakati barani Afrika inayoendeleza uongozi wa wanawake, afya, elimu, na ushirikishwaji wa kiuchumi.

Rachel Ruto na Rais William Ruto wana watoto 6 pamoja na binti mmoja waliyemuasili mwaka wa 2015.

CHANZO:TRT Swahili