Idadi ya vifo vilivyotokana na ugonjwa wa virusi vya Ebola sasa vimevuka 900, kulingana na kanzi data iliyotolewa siku ya Jumatatu.
Kulingana na takwimu ya Wizara ya Afya ya nchi hiyo, idadi ya maambukizi imefikia 2,344, vikiwemo vifo 930.
Wizara hiyo, imeongeza kuwa, wagonjwa wapatao 724 wamewekwa chini ya uangalizi maalumu, huku 466 wakipona kabisa ugonjwa huo.
Maeneo yaliyoathirika zaidi ni pamoja na Haut-Uele, Ituri, Kivu Kaskazini, Kivu Kusini na Tshopo.
Kwa upande wake, Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC), kimesema kuwa kuendelea kutuma timu za wahudumu wa afya, kuhakikisha kuwa ugonjwa huo unadhibitiwa.
CHANZO:Anadolu Agency











