| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
WHO yatangaza mgonjwa wa kwanza kupona mlipuko wa Ebola DRC
Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema kupona kwa mgonjwa huyo ni kutokana na kutambua mapema, kutenga watu na kutoa matibabu ya haraka kunachangia kwa mtu kupona.
WHO yatangaza mgonjwa wa kwanza kupona mlipuko wa Ebola DRC
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekumbwa na milipuko kadhaa ya Ebola. / Reuters

Shirika la Afya Duniani siku ya Ijumaa lilitangaza kupona kwa mgonjwa wa kwanza wa mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

"DRC imesema kuwa Mei 27, mgonjwa mmoja alipata nafuu na kuondoka hospitali na amejumuika na jamii tayari," Afisa wa WHO Anais Legand amewaambia waandishi wa habari, akiongeza kuwa "alikuwa wa kwanza".

Kulingana na WHO, mgonjwa huyo aliruhusiwa kuondoka hospitali baada ya vipimo vya maabara kuthibitisha kuwa hana tena virusi. Kupona huku kunaonekana kuwa dalili nzuri kwa wahudumu wa afya wanaokabiliana kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.

Bundibugyo strain

Mlipuko huu wa sasa wa virusi aina ya Bundibugyo vya Ebola, umezua wasiwasi kwa mamlaka za afya za kikanda na kimataifa.

Maafisa wa WHO wanasema kupona kwa mgonjwa huyo kunaashiria uangalizi wa mapema, kutenga wagonjwa na kutoa msaada wa matibabu kunaweza kusaidia katika mgonjwa kupona.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekumbwa na milipuko kadhaa ya Ebola katika kipindi cha miongo kadhaa.

Maafisa wa afya wanaendelea kufuatilia maambukizi yanayosemekana kuwa ni ya Ebola katika mikoa ya karibu na nchini jirani.

Ghebreyesus yuko nchini DRC

Mkuu wa WHO, ambaye yuko DRC kusaidia kukabiliana na mlipuko wa Ebola, alitarajiwa kukutana na mamlaka za DRC siku ya Ijumaa kabla ya kwenda kwenye kitovu cha mlipuko huo siku ya Jumamosi.

Tedros Adhanom Ghebreyesus aliwasili mji mkuu, Kinshasa, Alhamisi jioni, wiki mbili baada ya mlipuko huo unaoambukiza kwa haraka kutangazwa.

CHANZO:TRT Afrika and agencies