Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki, amepongeza Mkutano wa 31 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31) uliondaliwa na Uturuki, akiulezea kuwa wa mafanikio kihistoria katika maandalizi na mahudhurio yake.
Erdogan ametoa kauli hiyo wakati akihutubua mkutano wa vijana wa chama cha AK, uliofanyika jiini Ankara siku ya Jumatatu.
Akizungumzia mkutano mwingine wa NATO uliofanyika jijini Ankara mwezi Julai, Erdogan alisema mkutano huo unaendelea kuwa na faida hadi kufikia sasa.
“Bado tunaendelea kuona faida za mkutano huo. Faida zake zinaonekana ulimwenguni mzima,” alisema.
Akigusia ushawishi wa Uturuki ambao unaendelea kuongezeka, Erdogan alisema kuwa nchi hiyo itaendelea kutilia mkazo suala la elimu duniani, huku miradi ya ndani ikiendelea kuvutia macho na masikio duniani.
"Kadiri mfumo mpya wa dunia unavyojitokeza, ni nyinyi ambao mtaifanya Uturuki kuwa kitovu cha kila uhalisia," alisema Erdogan wakati akiwahutubia vijana hao.





















