| Swahili
ULIMWENGU
2 dk kusoma
Kanisa Katoliki lajitenga na Jumuiya ya Mtakatifu Pius wa 10
Jumuiya ya Mtakatifu Pius X yenye wafuasi wapatao 600,000 ulimwenguni, inapinga vikali mabadiliko ya kisasa yaliyoletwa na Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican wa mwaka 1962-65, imeweka msisitizo kwenue matumizi ya Misa ya kale ya Kilatini.
Kanisa Katoliki lajitenga na Jumuiya ya Mtakatifu Pius wa 10
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV./Picha:Reuters

Makao Makuu ya Kanisa Katoliki duniani, Vatican imetangaza kujitenga na Jumuiya ya Mtakatifu Pius X (SSPX), baada ya jumuiya hiyo kuwasimika maaskofu wanne bila idhini ya Papa Leo XIV.

Hatua hiyo, inawalenga maaskofu wapya wanne, Wafaransa wawili, Mmarekani raia wa Uswisi.

Kulingana na Vatican, uamuzi unaochukuliwa kama uasi ndani ya Kanisa hilo lenye waumini wapatao Bilioni 1.42 duniani.

Vatican imeongeza kuwa, Baraza la Kipapa la Mafundisho ya Imani limetangaza kuwa maaskofu, mapadri, na hata waumini wanaofuata jumuiya hiyo wamejitenga rasmi na Kanisa Katoliki.

Hali kadhalika, Vatican imewatadhaharisha waumini Wakatoliki kuhusu Sakramenti zitolewazo na jumuiya hiyo, ikiwemo Kitubio na Ndoa, kuwa ni batili na hazihesabiki kuwa halali ndani ya kanisa hilo.

Jumuiya ya Mtakatifu Pius X yenye wafuasi wapatao 600,000 ulimwenguni, inapinga vikali mabadiliko ya kisasa yaliyoletwa na Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican wa mwaka 1962-65, imeweka msisitizo kwenue matumizi ya Misa ya kale ya Kilatini, huku wakiishutumu Vatican kwa uhuru mkubwa wa kidini na mabadiliko.

Mgogoro huu umedumu kwa miongo kadhaa tangu jumuiya hiyo ilipoanzishwa mwaka 1970. Licha ya jitihada za muda mrefu za maridhiano zilizofanywa na Mapapa waliotangulia, maamuzi ya jumuiya hiyo iliyoanzishwa mwaka 1970,  ya kuendelea kuweka wakfu viongozi bila idhini ya Vatican yamesababisha mgogoro mkubwa na Vatican.

 

CHANZO:AFP