| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Rais Zelenskyy wa Ukraine ‘atenga’ siku 40 za kuishambulia Urusi
Hata hivyo, kiongozi huyo hakutoa taarifa zaidi kuhusu namna operesheni hiyo itakavyoendeshwa.
Rais Zelenskyy  wa Ukraine ‘atenga’ siku 40 za kuishambulia Urusi
Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine./Picha:Wengine / Others

Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine amesema kuwa ameidhinisha operesheni ya siku 40 yenye kuiongezea shinikizo na kuishambulia Urusi.

Katika taarifa yake ya Alhamisi aliyoichapisha kwenye mtandao wa Telegram, Zelenskyy alibainisha kuwa, alipokea ripoti kutoka kwa Meja Jenerali Yevhen Khmara kuhusu mipango ya nchi yake kutumia makombora ya masafa marefu na ya kati pamoja na shughuli zingine za Idara ya Ulinzi na Usalama cha Ukraine (SBU) kupitia kituo chake cha operesheni, kijulikanacho kama Alpha.

"Nimeidhinisha siku 40 za Idara ya Usalama kwa nia ya kuongeza mashambulizi ili hatimaye vita hivyi vifike mwisho," alisema Zelenskyy kupitia ujumbe huo wa Telegram.

Hata hivyo, kiongozi huyo hakutoa taarifa zaidi kuhusu namna operesheni hiyo itakavyoendeshwa.

Kwa upande mwingine, Zelenskyy alisifu uwezo na ufanisi wa SBU katika uwanja wa mapambano, akibainisha kuwa idara hiyo imepata mafanikio makubwa katika kuilinda, hususani kupitia matumizi ya droni za kivita.

Kulingana na Zelenskyy, operesheni maalumu ya Alpha, imegeuka kinara katika mashambulizi dhidi ya Urusi na vifaa vyao.

 

 

CHANZO:AA