| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Rais wa Chama cha Soka cha Palestina agoma kumsalimia mwenzake wa Israel wakati wa mkutano wa FIFA
Tukio hilo lilitokea siku ya Alhamisi, wakati wa Mkutano Mkuu wa 76 wa FIFA mjini Vancouver, Canada, mara tu baada ya rais wa FIFA Gianni Infantino kumuomba Rajoub amsalimu Bassem Sheikh Suleiman, ambaye ni Makamu Rais wa soka wa Israel.
Rais wa Chama cha Soka cha Palestina agoma kumsalimia mwenzake wa Israel wakati wa mkutano wa FIFA
Rais wa Chama cha Soka cha Palestina Jibril Rajoub, amegoma kupeana mkono na rais mwenzake kutoka Israel./Picha:Wengine

Rais wa Chama cha Soka cha Palestina Jibril Rajoub, amegoma kupeana mkono na rais mwenzake kutoka Israel, akisema kuwa “heshima ya taifa lake, haitozingatia itifaki”.

Tukio hilo lilitokea siku ya Alhamisi, wakati wa Mkutano Mkuu wa 76 wa FIFA mjini Vancouver, Canada, mara tu baada ya rais wa FIFA Gianni Infantino kumuomba Rajoub amsalimu Bassem Sheikh Suleiman, ambaye ni Makamu Rais wa soka wa Israel.

Muda mfupi baada ya tukio hilo, Rajoub alisambaza picha mjongeo kupitia mtandao wa Facebook, iliyokuwa na ujumbe uliosomeka:

“Tulionesha wazi msimamo wetu kwenye jukwaa la FIFA kwa kukataa kupeana mkono na mwakilishi kutoka shirikisho la soka la Israel.”

Rajoub alisisitiza kuwa, ishara hiyo ni ukumbusho kuwa, heshima ya taifa la Palestina haitoangalia wala kuzingatia itifaki mahali husika.

Aliongeza kuwa, chama cha soka cha Palestina kitakata rufaa katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kufuatia uamuzi wa FIFA wa kutochukua hatua zozote kuhusu ukiukwaji wa haki uliofanywa na klabu za mpira wa miguu za Israel, kwenye maeneo yanayokaliwa kimabavu.

Kulingana na Rajoub, rufaa rasmi iliwasilishwa Aprili 22, 2026, kwa lengo la “kukata mzizi wa fitina” na kuhakikisha kuwa sheria zinafuata mkondo wake, hasa katika tasnia ya michezo.

CHANZO:AA