| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Rais Trump abadilisha jina la Hormuz na kuwa 'Strait of Trump'
Rais wa Marekani Donald Trump amechapisha ramani kwenye mtandao wake wa kijamii Truth Social ikionyesha Strait of Hormuz ikiwa imepewa jina la “Strait of Trump,” badala ya jina lake rasmi la Strait of Hormuz, maarufu Mlango Bahari wa Hormuz.
Rais Trump abadilisha jina la Hormuz na kuwa 'Strait of Trump'
Mlango huo wa bahari ni mojawapo ya njia muhimu zaidi za usafirishaji wa mafuta duniani./ / Wengine

Mlango huo wa bahari ni mojawapo ya njia muhimu zaidi za usafirishaji wa mafuta duniani, huku mgogoro wa Marekani na Iran ukiwa bado unaendelea.

Wachambuzi wamelitafsiri tukio hilo kama ujumbe wa kisiasa au wa kuamsha mjadala, unaoendana na mtindo wa Trump wa kutumia kauli zenye mvuto mkubwa wakati wa hali za mvutano wa kisiasa.

Hii si mara ya kwanza Trump kwa kutoa kauli kama hiyo. Katika taarifa ya awali, alionekana kuchanganya jina hilo, akisema Iran inahitaji "kufungua Mlango wa Trump, hapo hapo akaghairi na kusema kuwa alimaanisha Hormuz."

CHANZO:TRT Afrika