| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Aliyejaribu kumuua Donald Trump kupandishwa mahakamani
Mshukiwa huyo, ambaye alikuwa amejihami kwa bunduki mbili na kisu, alikuwa akiishi kwenye hoteli ya Washington Hilton, eneo ambalo hafla hiyo ilikuwa ikifanyika.
Aliyejaribu kumuua Donald Trump kupandishwa mahakamani
Cole Allen akiwa chini ya ulinzi wa maafisa usalama wa Marekani./Picha:Reuters / Reuters

Mshukiwa wa jaribio la kumuua Rais Donald Trump wa Marekani anatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Jumatatu.

Cole Allen, mwenye umri wa miaka 31, anatarajiwa kupandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza siku ya Jumatatu, akishtakiwa kwa kosa la kufanya shambulizi dhidi ya ofisa wa usalama kwa kutumia bunduki.

Mshukiwa huyo, ambaye alikuwa amejihami kwa bunduki mbili na kisu, alikuwa akiishi kwenye hoteli ya Washington Hilton, eneo ambalo hafla hiyo ilikuwa ikifanyika.

Mkazi huyo wa California alitiwa nguvuni, muda mfupi baada ya majibizano ya risasi na walinda usalama wakati wa hafla  ya wanahabari iliyoandaliwa na Rais Trump, siku ya Jumamosi.

Tukio hilo linakuwa jaribio la tatu la kuutoa uhai wa Trump, ndani ya miaka miwili.

Katika mahojiano yake na kituo cha CBS, Jumapili usiku, Trump alisisitiza kuwa hahofii chochote mara baada ya tukio hilo, akisema kuwa anatambua kuwa anaishi katika ulimwengu wa ajabu.