| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Huduma za usafirishaji zapungua Mlango Bahari wa Hormuz baada ya mashambulizi ya meli za mizigo
Licha ya mashambulizi hayo, meli kadhaa zimeendelea kuvuka katika lango hilo maarufu duniani.
Huduma za usafirishaji zapungua Mlango Bahari wa Hormuz baada ya mashambulizi ya meli za mizigo
Licha ya mashambulizi hayo, meli kadhaa zimeendelea kuvuka katika lango hilo maarufu duniani./Picha:@themaritimenet / Others

Huduma za usafiri wa meli za mizigo katika Mlango Bahari wa Hormuz zimeendelea, japo kwa kasi ndogo kufuatia kushambuliwa kwa meli mbili hivi karibuni.

Kanzi data ya hali ya usafirishaji katika eneo, ilionesha shughuli za usafiri zikiendelea, japo kwa kasi ndogo, kufuatia kushambuliwa kwa vyombo viwili vya wa Ever Lovely na M/T Kiku.

Kulingana na Mamlaka ya Bandari ya Singapore, chombo cha Ever Lovely kilipata madhara madogo kufuatia kushambuliwa Juni 25 wakati likitoka katika Mlango Bahari wa Hormuz.

Kwa mujibu wa Kamanda Kuu ya Marekani, majeshi ya Iran, yalifanya shambulizi la droni kwenye meli ya M/T Kiku, ambayo ilikuwa na shehena ya zaidi ya mapipa milioni mbili ya mafuta ghafi.

Licha ya mashambulizi hayo, meli kadhaa zimeendelea kuvuka katika lango hilo maarufu duniani.

CHANZO:AA