| Swahili
ULIMWENGU
2 dk kusoma
Misri, Uturuki na Pakistan katika jitihada za upatanishi: Vyombo vya habari Marekani
Iran imesema haitaki kusitishwa kwa mapigano kwa muda, bali kusitishwa kabisa kwa mapigano katika kanda
Misri, Uturuki na Pakistan katika jitihada za upatanishi: Vyombo vya habari Marekani
Wapatanishi wanajaribu kukubaliana katika vipengele vitakavyojenga imani na kuleta pande zote mbili kukutana. / AP
tokea masaa 20

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Uturuki na Pakistan wanashughulikia mazungumzo kati ya Iran na Marekani, vyombo kadhaa vya habari nchini Marekani vimeripoti mwishoni mwa juma.

Mawaziri hao kutoka nchi tatu wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu kwa wakati tofauti na Waziri wa Mambo wa Nje wa Iran Araghchi na mjumbe wa Rais wa Marekani Donald Trump Steve Witkoff mwishoni mwa juma, lakini hakuna makubaliano yaliyofikiwa, kwa mujibu wa jarida la Wall Street Journal na Axios.

Axios imenukuu vyanzo viwili vilivyoshiriki katika majadiliano, ambavyo vimesema mazungumzo yanafanyika kupitia wapatanishi kutoka Pakistan, Misri na Uturuki lakini pia kupitia ujumbe mfupi unaotumwa mara kwa mara kati ya mshauri wa Trump na Araghchi.

Araghchi awali alisema mawasiliano na Marekani sio sehemu ya majadiliano lakini yanaishia katika kutumiana ujumbe, aidha moja kwa moja au kupitia wapatanishi.

Usitishwaji wa mapigano kwa muda?

Maafisa nchini Iran wamekataa kulegeza matakwa yao na wamekataa pendekezo la kufungua Mlango Bahari wa Hormuz kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda, kwa mujibu wa Jarida la Wall Street.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alisema siku ya Jumanne kuwa Iran haitaki usitishwaji wa mapigano wa muda bali inataka kusitishwa kabisa kwa mapigano katika eneo hilo.

Wapatanishi wanajaribu kukubaliana katika vipengele vitakavyojenga imani ambavyo vinaweza kusogeza mbele muda uliowekwa na Trump na kuzikutanisha pande zote mbili.

Trump ameweka Jumanne usiku siku ya mwisho ya kufunguliwa kwa Mlango Bahari wa Hormuz, akitahadharisha kwamba Iran itapoteza kila kinu cha nishati na miundombinu mikubwa ya nchi.

Marekani na Israel wameishambulia Iran tangu Februari 28, na kuua zaidi ya watu 1,340, ikiwemo Kiongozi Mkuu Ali Khamenei.

Iran imerudishia kwa mashambulizi katika nchi za Ghuba na kuzuia usafiri kupitia Mlango Bahari wa Hormuz, na kutatiza usafirishaji wa takriban mapipa ya mafuta milioni 20 kwa siku, hivyo kutatizo soko la dunia.