Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV ataikosa ziara yake ya Assisi wiki ijayo, kwa ushauri wa daktari, siku chache baada ya kufanyiwa upasuaji wa mapafu.
Kulingana na Vatican, ziara ya Papa Leo XIV ya kuelekea Assisi kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 40 siku ya maombezi ya Mtakatifu Paulo wa II kuhusu Amani Duniani, sasa imeahirishwa kwa ushauri wa madaktari.
Katika taarifa hiyo, Vatican imesema kuwa Papa Leo XIV, ameshauriwa asisafiri sehemu yoyote, hivyo atashiriki kumbukizi hiyo kwa kutuma ujumbe maalumu kwa washiriki wa tukio hilo.
Ziara hiyo ya mji wa Assisi, ni ishara ya kumbukizi ya mjumuiko wa kiimani, ambao uliandaliwa na Mtakatifu Yohanne Paulo wa II, mwaka 1986.
Vatican imesisitiza kuwa, shughuli zote za kiongozi huyo, sasa zitafuata ushauri na maelekezo ya madaktari wakati anapoendela kupona baada ya upasuaji wake.























