| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Uturuki yatuma salamu za rambirambi Misri kufuatia ajali ya treni
Abiria saba walifariki dunia na wengine 112 walijeruhiwa baada ya mabehewa kadhaa ya treni ya abiria kutoka kwenye njia ya reli na kupinduka katika mkoa wa Giza, kulingana na wizara ya afya.
Uturuki yatuma salamu za rambirambi Misri kufuatia ajali ya treni
"Tunamuomba Mwenyezi Mungu awarehemu wale waliopoteza maisha, na tunawatakia nafuu ya haraka majeruhi."

Uturuki imetuma salamu za rambirambi kwa nchi ya Misri kufuatia ajali ya treni iliyotokea Jumapili katika mkoa wa Giza, na kusababisha vifo vya watu saba huku wengine 112 wakijeruhiwa.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imesema imesikitishwa sana na vifo vilivyotokana na ajali hiyo iliyotokea Novemba 8 katika mkoa wa Giza, nchini Misri.

Katika taarifa rasmi iliyotolewa Jumatatu, wizara hiyo ilieleza: “Tumesikitishwa sana na vifo vilivyotokana na ajali ya treni iliyotokea jana (Novemba 8) katika mkoa wa Giza, nchini Misri. Tunawaombea marehemu wapumzike kwa amani, tunatoa pole kwa familia zao na kwa wananchi wa Misri, na tunawatakia majeruhi wote nafuu ya haraka.”

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Misri, watu saba walifariki dunia na wengine 112 kujeruhiwa baada ya mabehewa kadhaa ya treni ya abiria kutoka kwenye njia ya reli na kupinduka katika mkoa wa Giza, kaskazini mwa Misri.

Ajali hiyo ilitokea karibu na kijiji cha Gerza, katika wilaya ya Al-Ayyat, kando ya njia ya reli ya Cairo–Aswan.

Shirika la Reli la Taifa la Misri lilieleza kuwa treni namba 134, iliyokuwa ikisafiri kutoka Giza kuelekea Fayoum, iligongana na treni namba 2010 iliyokuwa ikisafiri kutoka Cairo kuelekea Aswan.

Tukio hilo lilitokea kati ya vituo vya Kafr Ammar na Al-Riqqa na kusababisha mabehewa kadhaa ya treni hiyo kutoka kwenye reli.

CHANZO:َAA