Taifa la Uingereza limeshuhudia Mawaziri Wakuu sita wakiingia na kutoka madarakani, lakini paka maarufu nchini humo Larry bado anaendelea kuishi katika makazi rasmi ya Waziri Mkuu wa Uingereza, 10 Downing Street.
Hadi kufikia sasa, Mawaziri Wakuu sita wa Uingereza wameingia na kutoka madarakani, lakini Paka maarufu nchini humo Larry bado anaendelea kuishi katika makazi rasmi ya Waziri Mkuu wa Uingereza, 10 Downing Street.
Paka huyo mwenye miaka 19, ameshuhudia utawala wa Mawaziri Wakuu sita wa Uingereza, ndani ya kipindi cha miaka 15.
Kimsingi, paka huyu ameishi ndani ya makazi na ofisi ya waziri mkuu wa kwa miaka yote hiyo, akishuhudia utawala wa David Cameron, Theresa May, Boris Johnson, Liz Truss, Rishi Sunak na hatimaye Keir Starmer, ambaye alijiuzulu Juni 22, mwaka huu.
Larry alihamia katika makazi hayo Februari 2011, chini ya uongozi wa David Cameron baada ya kuokotwa kutoka makazi ya wanyama yajulikanayo kama Battersea Dogs & Cats Home, kwa lengo la kupambana na tatizo la panya na ndani ya 10 Downing Street.
Hata hivyo, tofauti na wanasiasa wanaoingia na kutoka katika jengo hilo maarufu lenye mlango mweusi, Larry si mali ya Waziri Mkuu.
Yeye, anafanya kazi chini ya Ofisi ya Baraza la Mawaziri, jambo linalomaanisha kuwa majukumu yake yanaendelea bila kujali nani anayeongoza serikali.
Umaarufu wa paka Larry umeendelea kuvuka mipaka ya Uingereza, kiasi cha kujitokeza kwenye matukio makubwa ya kisiasa na hata kuonekana akicheza na Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama na Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine.
Kwa sasa paka huyu atakuwa anasubiri kumpokea mrithi wa Keir Starmer ndani ya mjengo wa 10 Downing Street, huku akiendelea na ukamataji panya.












