| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Balozi za Marekani Ulaya zatoa tahadhari ya usalama kipindi cha msimu wa sikukuu
Tahadhari hiyo imetolewa dhidi ya mikusanyiko ambayo “ inaweza kuonekana kama fursa ya makundi ya kigaidi na wahalifu.”
Balozi za Marekani Ulaya zatoa tahadhari ya usalama kipindi cha msimu wa sikukuu
Raia wa Marekani wametakiwa kuchukua tahadhari za kiusalama wakati msimu wa sikukuu unapokaribia / АА

Balozi za Marekani zilizopo Ulaya zimetoa tahadhari ya usalama ya pamoja kwa raia wake kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa tishio la kiusalama wakati msimu wa sikukuu unapokaribia.

“Raia wa Marekani wanatakiwa kuwa na tahadhari katika mazingira yao na tahadhari binafsi ya kiusalama,” umesema Ubalozi wa Marekani jijini London katika taarifa ambayo inahusu Uingereza na Ulaya kwa ujumla.

Tahadhari hiyo imetolewa dhidi ya mikusanyiko ambayo “ inaweza kuonekana kama fursa ya makundi ya kigaidi na wahalifu.”

Maeneo yanayoweza kulengwa ni pamoja na sehemu za watalii kama vile masoko, vituo vya usafiri, maduka makubwa, sehemu za ibada na maeneo mengine ya umma, imesema taarifa hiyo.