| Swahili
MICHEZO
2 dk kusoma
Madada wawili wa Malawi kuendelea kuibeba timu fainali za WAFCON dhidi ya Cameroon
Timu ya taifa ya wanawake ya Malawi imefanikisha kile wengi wataona kuwa jambo ambalo halikuwa linawezekana.
Madada wawili wa Malawi kuendelea kuibeba timu fainali za WAFCON dhidi ya Cameroon
Mchezaji wa Malawi Tabitha Chiwenga anavaa jezi nambari 11, huku dada yake Temwa akivaa jezi nambari 10.

Timu ya taifa ya wanawake ya Malawi imefanikisha kile wengi wataona kuwa jambo ambalo halikuwa linawezekana.

Katika mashindano yake ya kwanza WAFCON, wamefika hadi fainali.

Wamewafunga Algeria 3-1 kwenye nusu fainali mji mkuu wa Morocco, Rabat siku ya Jumatano, Agosti 12, na sasa itakabiliana na Cameroon kwenye fainali. Cameroon iliwashangaza wenyeji Morocco kwa kuwafunga mikwaju ya penati 3-1 kufuatia mechi kumalizika bila kufungana muda wa ziada.

Kihistoria, Cameroon ni timu yenye uwezo mkubwa WAFCON. Wameshiriki mashindano hayo mara 13, mara tatu ikimaliza katika nafasi ya pili mwaka 2004, 2014, na 2016. Katika fainali zote hizo walishindwa na Nigeria.

Kiatu cha dhahabu

Katika mechi nyingine ya nusu fainali ya WAFCON 2026, magoli yote matatu ya Malawi dhidi ya Algeria yalifungwa na madada wawili – Temwa Chawinga mwenye umri wa miaka 27 na Tabitha Chawinga, mwenye umri wa miaka 30 (aliyefunga magoli mawili).

Tabitha, ambaye anavaa jezi nambari 11, ni nahodha wa timu hiyo ya taifa ya wanawake, ilhali Temwa, ambaye anavaa jezi nambari 10, ni nahodha msaidizi.

Ndugu hao wote wanafukuzia kushinda kiatu cha dhahabu. Temwa anaongoza akiwa na magoli matano, sawa na Barbra Banda wa Zambia. Tabitha amefunga jumla ya magoli manne, huku fainali ikitatarajiwa siku ya Jumapili, Agosti 16.

Tabitha anacheza kwenye klabu ya Ufaransa ya Olympique Lyonnais, ilhali Temwa akiwa na timu ya Kansas City nchini Marekani.

Rais wa Malawi ana matumaini ya ushindi

Timu zote mbili Malawi na Cameroon zitakuwa zinawania kushinda kombe la WAFCON kwa mara ya kwanza katika historia.

Timu tatu pekee ndizo ambazo zimeshinda taji la WAFCON kufikia sasa, ni Nigeria (mara 10), Equatorial Guinea (mara mbili), na Afrika Kusini (mara moja).

Je, Malawi itafanikiwa kuishinda Cameroon katika fainali ya siku ya Jumapili?

Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika ana matumaini ya ushindi, akisema Jumatano: "Sasa hivi, dakika 90 tu ndiyo ziko kati yetu na Kombe la Mashindano ya soka ya Mataifa ya Afrika kwa wanawake."

CHANZO:TRT Afrika