Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, ameweka wazi nia yake ya kuiunga mkono Urusi, hususani katika uwanja wa vita.
Kim alitoa hakikisho hilo, kupitia ujumbe alioutuma kwa siku ya Jumapili, kwa Rais Vladimir Putin, kama majibu ya pongezi alizotoa Putin kwa Kim, katika sherehe ya kutimiza miaka 78 ya kuanzishwa kwa Korea Kaskazini, kulingana na chombo cha habari cha nchi hiyo, (DPRK).
“Tukiaminishwa na ushindi wa Urusi katika mapambano mbalimbali huko nyuma, ninatoa ahadi ya kukuunga mkono ndugu yangu na Warusi wote kwa ujumla,” alisema Kim.
Kulingana na Kim, Korea Kaskazini na Urusi zilikuwa zinaandika historia mpya ya ushirikiano, kwa kulinda mataifa hayo mawili.
Kim aliongeza kuwa, nchi yake itaendelea kushirikiana na kukuza ushirikiano na Urusi.
Ushirikiano kati ya mataifa hayo, umeendelea kuongezeka tangu mataifa hayo yalipokubaliana kushirikiana, mwezi Juni 2024.
Makubaliano, yanahusisha zaidi ushirikiano katika nyanja za kiulinzi.




















