Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz, ameonya kwamba Israel "itamuangamiza" kiongozi yeyote wa Iran atakayepanga au kujaribu kuishambulia nchi hiyo.
Kauli yake imekuja wakati maelfu ya watu wamejitokeza jijini Tehran siku ya Jumatatu kushiriki kuomboleza aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Iran, Ali Khamenei, ambaye inadaiwa aliuawa katika shambulio la pamoja la Marekani na Israel tarehe 28 Februari.
"Kiongozi yeyote wa Iran atakayejaribu tena kuendeleza mipango ya kuiangamiza Israel pia ataangamizwa," Katz alisema katika taarifa iliyonukuliwa na gazeti la The Jerusalem Post.
Aidha, alidai kuwa mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran "yaliondoa tishio la haraka la kuangamizwa kwa Israel na kuharibu kwa kiwango kikubwa uwezo wa kimkakati wa Iran."















