| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Mali yaripoti mashambulizi mapya ya kigaidi katika miji mikuu.
Mashambulizi hayo yaliripotiwa katika miji ya kaskazini ya Gao, Anefis na Aguelhok, pamoja na mji wa kati wa Sevare na gereza la Kenieroba karibu na mji mkuu, Bamako.
Mali yaripoti mashambulizi mapya ya kigaidi katika miji mikuu.
Askari wa Mali akiwa ameshika doria wakati wa shambulio dhidi ya kambi kuu ya kijeshi ya Mali Bamako, mnamo Aprili 2026. / Reuters / Reuters

Jeshi la Mali lilisema Jumamosi kuwa miji kadhaa kaskazini mwa nchi hiyo, ikiwemo miji mikubwa ya Gao na Sévaré, ilishambuliwa na magaidi.

Mapigano hayo, yaliyoanza majira ya saa kumi na moja alfajiri , yalitokea ikiwa imepita miezi miwili na ushei tangu kundi la kigaidi lenye uhusiano na Al-Qaeda, likishirikiana na waasi wanaotaka kujitenga wanaoongozwa na kabila la Tuareg, lilipofanya mashambulizi yaliyosababisha kifo cha Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo.

Mashambulizi hayo mapya yaliripotiwa katika miji ya kaskazini ya Gao, Anefis na Aguelhok, pamoja na mji wa kati wa Sevare na gereza la Kenieroba karibu na mji mkuu, Bamako.

Mkazi mmoja wa Anefis aliambia shirika la habari la AFP kuwa "makundi yenye silaha yapo mjini humo, lakini jeshi bado linapambana. Kambi (iliyopo hapo) bado haijatekwa".

Uwepo wa jeshi

Miji ya Anefis na Aguelhok ndiyo maeneo ya mwisho ambapo jeshi la Mali bado linadhibiti maeneo katika eneo la Kidal, kaskazini mwa nchi, kufuatia mashambulizi ya mwezi Aprili.

Huko Gao, pia kaskazini mwa nchi, wakazi waliambia AFP kuhusu milio ya risasi na "milipuko mikubwa" karibu na kambi ya jeshi.

Katika mji wa kati wa Sevare, "milipuko ilisikika... majira ya saa 11 alfajiri, ingawa chanzo chake bado hakijajulikana. Muda mfupi baadaye, ndege kadhaa zilionekana zikiruka juu ya eneo hilo," chanzo cha usalama kiliambia AFP.

Gereza la Kenieroba, ambako magaidi na wafungwa wengine wanazuiliwa, pia lilishambuliwa; gereza hilo liko umbali wa takriban kilomita 70 kusini-magharibi mwa Bamako.

‘Chini ya vitanda vyetu’

“Tuko chini ya vitanda vyetu, milio ya risasi inaendelea,” mfungwa mmoja aliiambia AFP, kabla mawasiliano hayajaonekana kukatika.

Kituo Kikuu cha Kenieroba ndicho kituo kikubwa zaidi cha kisasa cha adhabu nchini Mali, chenye uwezo wa wafungwa zaidi ya 2,500.

Serikali inayoongozwa na Assimi Goita inapambana na mashambulizi ya washirika wa Afrika Magharibi wa Al-Qaeda na makundi ya kigaidi ya Daesh. Pia inapambana na historia ndefu zaidi ya utengano unaoongozwa na Tuareg kaskazini.

CHANZO:TRT Afrika and agencies