| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Rais wa Uturuki Erdogan amempokea Waziri Mkuu wa Pakistan Sharif mjini Istanbul
Ujumbe wa ngazi ya juu kutoka Uturuki na Pakistan unatarajiwa kukutana kufuatia mazungumzo ya pande mbili.
Rais wa Uturuki Erdogan amempokea Waziri Mkuu wa Pakistan Sharif mjini Istanbul
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akutana na Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif Istanbul, turuki Julai 04, 2026. / AA / AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan siku ya Jumamosi alimpokea Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif katika Ikulu ya Vahdettin mjini Istanbul.

Kufuatia hafla ya mapokezi rasmi viongozi hao wawili waliendelea na mkutano baina ya nchi hizo mbili.

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Hakan Fidan, mkuu wa Shirika la Kitaifa la Ujasusi Ibrahim Kalin, Mkuu wa Mawasiliano Burhanettin Duran, na mshauri mkuu wa rais Akif Cagatay Kilic walihudhuria mkutano huo wa faragha.

Kufuatia mkutano huo wa pande mbili, viongozi hao wanatarajiwa kufanya mkutano wa ngazi ya wajumbe.

Erdogan na Sharif pia watafanya mkutano wa pamoja wa wanahabari.

CHANZO:AA