| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Uingereza yasitisha mazoezi yake ya kijeshi Kenya baada ya kunyimwa leseni
Kupitia taarifa yake ya Alhamisi, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilioneshwa kusikitishwa na maamuzi hayo, ikisisitiza kuwa itaendelea kudumisha uhusiano mwema na Kenya.
Uingereza yasitisha mazoezi yake ya kijeshi Kenya baada ya kunyimwa leseni
Mazoezi hayo ya wiki sita, yaliyopewa jina la Haraka Storm, yalipangwa kufanyika katika Kaunti ya Laikipia, iliyopo kilomita 200 kutoka Nairobi.

Uingereza imesitisha kufanya mazoezi ya kijeshi yaliyokuwa yafanyike baada mwaka huu nchini Kenya, baada ya mamlaka za nchi hiyo kuinyima leseni.

Kupitia taarifa yake ya Alhamisi, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilioneshwa kusikitishwa na maamuzi hayo, ikisisitiza kuwa itaendelea kudumisha uhusiano mwema na Kenya.

"Bado tunathamini mahusiano na Kenya. Mazoezi yetu ya pamoja, yameendelea kuzifanya Kenya na Uingereza kuendelea kuwa salama," ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Mazoezi hayo ya wiki sita, yaliyopewa jina la Haraka Storm, yalipangwa kufanyika katika Kaunti ya Laikipia, iliyopo kilomita 200 kutoka Nairobi.

Uingereza imeweka kambi nchini kupitia kituo cha BATUK, ambako maelfu wa wanajeshi wa Uingereza hufanya mazoezi ya pamoja na wale wa Kenya.

Hata hivyo, baadhi ya wanasiasa wa Kenya wametaka baadhi ya wanajeshi wa Uingereza, kuchukuliwa hatua kutokana na vitendo vyao kwa jamii zilizo karibu na kambi zao.

CHANZO:Anadolu Agency