Beki wa Real Madrid na timu taifa ya Ujerumani, Antonio Rüdiger ametangaza rasmi kustaafu kuichezea timu yake ya taifa.
Uamuzi huo umefikiwa, baada ya beki huyo mwenye mbwembwe, kuitumikia timu ya taifa ya Ujerumani kwa miaka 12.
Rüdiger, ambaye ameichezea timu ya taifa ya Ujerumani mechi 86, amefikia uamuzi huo, ili kupisha wachezaji wachanga kuisaidia timu yao.
Antonio Rüdiger mwenye umri wa miaka 33 alianza kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani Mei 2014.
ZILIZOPENDEKEZWA
Ameshiriki katika mashindano matatu ya Kombe la Dunia (2018, 2022 na 2026). Aliwahi pia kucheza kwa timu za vijana wa taifa hilo lake.
CHANZO:TRT Afrika Swahili



















