Rais Donald Trump wa Marekani amekutana na maafisa watendaji wakuu wa makampuni ya gesi na mafuta ndani ya Ikulu ya White House siku ya Jumanne, kuzungumzia athari za vita vyake na Iran, hususani katika nishati.
Trump pamoja na wakuu hao, wamejadiliana hatua za kuchukua. iwapo Mlango Bahari wa Hormuz utaendelea kuwa umefungwa.
"Mara kwa mara, Rais amekuwa akikutana na wakuu hawa ili apate mrejesho kutoka kwao kutokana na hali ilivyo kwa sasa,” alisema ofisa mmoja wa Ikulu ya White kupitia taarifa yake siku ya Jumatano.
Kati ya waliohudhuria kikao hicho, ni pamoja na Waziri wa Nishati Scott Bessent, Mnadhimu Mkuu Susie Wiles na Makamu wa Rais wa Marekani, JD Vance.
Mbali na kujadili mustakabali wa Mlango Bahari wa Hormuz, pande hizo pia zilijadiliana uzalishaji wa ndani wa mafuta na hali halisi ya Venezuela.
Siku ya Jumatano, bei ya mafuta kwa lita ilifika Dola 4.229, kulingana na Chama cha Waendesha Magari nchini Marekani.













