| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Waandamanaji wanaopinga kujengwa kwa kituo cha Marekani cha Ebola wakamatwa nchini Kenya
Ujenzi wa kituo cha Ebola ulizuiwa kwa muda na Mahakama ya Juu nchini Kenya na pia umekuwa ukipingwa na wanasiasa wa nchi hiyo.
Waandamanaji wanaopinga kujengwa kwa kituo cha Marekani cha Ebola wakamatwa nchini Kenya
Waandamanaji wanapinga kituo cha karantini ya Ebola kitakachoanzishwa na Marekani katika Kambi ya Jeshi la Anga ya Laikipia mjini Nanyuki, Kenya. / AP

Wakenya kadhaa wamekamatwa Jumanne wakiwa katika maandamano ya kupinga ujenzi wa kituo cha Karantini cha Ebola kinachojengwa kwa ajili ya raia wa Marekani katika mji wa kitalii.

Kituo hicho, katika Kambi ya Jeshi la Anga ya Laikipia, mjini Nanyuki, katika eneo la Mlima Kenya, kitatumika kwa ajili ya karantini kwa raia wa Marekani wanaotoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ambayo hivi sasa inakabiliwa na mlipuko wa Ebola.

Mpaka sasa, Kenya bado haina rekodi yoyote ya mgonjwa wa Ebola, na wengi wanapinga wazo la kuleta watu wanaoshukiwa kuwa na ugonjwa ambao unaambukiza kwa kasi nchini mwao.

Mamia walikusanyika katika eneo la kambi hiyo, wengine wakiwa wamevaa zana za kujikinga huku baadhi wakiwa wamebeba majeneza yaliyoandikwa "Ebola."

‘Hatuna Ebola’

AFP imerekodi watu kadhaa waliokamatwa na polisi, ambao pia walirusha vilipuzi vya kutoa machozi kwa lengo la kutawanya vikundi vya watu.

Kituo hicho ambacho kimepangwa kuwa na vitanda 50 vilivyotengwa na kuendeshwa na wafanyakazi wa Marekani, kilifikia hatua za kukamilika mwishoni mwa juma.

Ujenzi ulisita baada ya Mahakama Kuu kuweka zuio la muda mfupi kufuatia malalamiko kutoka kwa wananchi na wanasiasa wa eneo hilo.

Hata hivyo, Rais William Ruto wa Kenya, serikali yake imesisitiza kuendelea na mpango huo, na kusema kuwa haitakuwa vyema kuikatalia Marekani ombi lake la kuweka kituo nchini humo.

Kwa nini Kenya 'haiwezi kukataa'

"Watu wa Marekani na serikali wamekuwa washirika wetu wa muda mrefu katika masuala ya afya kwa takriban miaka 25-30," amesema Rais Ruto wiki iliyopita.

"Itakuwa vibaya sana, iwapo ombi moja la Marekani la kuweka kituo kwa gharama zao, sisi tutakataa. Tutaonekana sio binadamu."

Waziri wa Afya nchini Kenya amesisitiza kwamba, Wakenya pia watatumia kituo hicho.

Marekani imeahidi kiasi cha fedha Dola milioni 13.5 kama sehemu ya jitihada za kukabiliana na Ebola.

Hatua hii inafutia makubaliano tata yaliyofikiwa miaka miwili iliyopita, ambapo Kenya ilikubali kutoa taarifa zake za afya kwa Marekani ikiwa ni mbadala wa msaada wa fedha.

Shirika la Afya Duniani limetangaza hali ya dharura ya kimataifa kutokana na mlipuko wa Ebola nchini DRC, ambapo wagonjwa 515 wamethibitishwa, ikiwemo vifo 91.

Licha ya hofu ya kuenea katika nchi jirani, ni Uganda pekee iliyorekodi maambukizi.

Mpaka sasa, wagonjwa 19 wamethibitishwa, wote wakiwa ni raia wa DRC waliovuka mpaka.

Soma zaidi
Rais wa Afrika Kusini aagiza hatua za kuwalinda wanawake kufuatia mfululizo wa mauaji
Misri yakana kuingilia mambo ya ndani ya Ethiopia na kuunga mkono makundi yenye silaha
Edward Kijanangoma atawazwa mfalme mpya wa Tooro
Je, Afrika itapata viti vya kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa?
Jeshi la Polisi Tanzania laonya wanaochochea mgomo wa madereva wa mabasi
Madaktari bingwa wa Tanzania waweka kambi ya matibabu Malawi
Makamu wa Rais Tanzania ataka vijana kupewa fursa za mafunzo ya ajira
Jeshi la Sudan lapinga madai ya kuunga mkono makundi ya upinzani Ethiopia
Uchaguzi Mkuu kurejesha utulivu Sudan Kusini?
Marekani italazimika kuondoka Mashariki ya Kati: Iran
Mashambulizi ya kigaidi mjini Mogadishu yapungua kwa karibu asilimia 90: Serikali ya Somalia
Maambukizi ya Ebola nchini DRC ni zaidi ya 8,000 tangu kuanza kwa mlipuko huo
Watoto 17 miongoni mwa wahamiaji 250 waliookolewa katika pwani ya Mauritania
Marekani kusitisha ufadhili wa sekta ya afya nchini Zimbabwe kufikia mwishoni mwa mwezi wa Septemba
Mwanamke wa kumi apatikana amefariki katika msururu  wa mauaji nchini Afrika Kusini
Qatar Airways yakopesha marubani kwa shirika la ndege la taifa la Rwanda
Wapiganaji wa RSF wahamia upande wa jeshi la Sudan baada ya kushuhudia 'maafa'
Mkuu wa Umoja wa Mataifa asikitishwa kwa kunyimwa viza  kiongozi wa Sudan, Burhan kuhudhuria UNGA
Jenerali wa DR Congo miongoni mwa watu 13 waliofariki katika ajali ya ndege
Afrika itapata hadhi ya uwanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa?