| Swahili
MICHEZO
2 dk kusoma
Mshambuliaji Aubameyang astaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Gabon
Mshambuliaji huyo wa Gabon amejiweka katika nafasi ambayo huenda akamalizia kucheza soka lake barani Ulaya.
Mshambuliaji Aubameyang astaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Gabon
Aubameyang anasema alidharauliwa na kuharibiwa sifa kutokana na timu yao kufungwa katika mashindano ya AFCON. / AA

Nahodha wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang ametangaza kuwa anajiuzulu kuichezea timu ya taifa lake, akisema kuwa anahisi "alidharauliwa" alipotengwa na baadaye kujumuishwa baada ya AFCON 2025 nchini Morocco.

 Mfungaji huyo bora katika historia ya 'the Panthers' alitajwa na serikali ya Gabon kama aliyechangia kwa matokeo mabaya ya timu yake ya taifa katika mashindano ya AFCON.

"Walitudhalilisha na kuniharibia sifa pamoja na kuwa nilicheza AFCON nikiwa na jeraha," alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 katika mahojiano kwenye televisheni.

"Huu ndio mwisho wangu, nadhani nimefika tamati sasa."

Matokeo mabaya AFCON

Gabon waliondolewa katika mashindano ya AFCON hatua ya makundi baada ya kufungwa mechi zote tatu, ya mwisho ikiwa dhidi ya Cote d’Ivoire.

"Ni sehemu ya utambulisho wa taifa letu ambayo imedhoofishwa," Rais wa Gabon Brice Clotaire Oligui Nguema alisema wakati huo.

Serikali ililitimua benchi lote la ufundi, ikasimamisha timu hiyo na kumuondoa Aubameyang na Bruno Ecuele Manga mwenye umri wa miaka 38.

Kumalizia soka lake Ulaya

Mshambuliaji huyo wa Gabon amejiweka katika nafasi ambayo huenda akamalizia kucheza soka lake barani Ulaya, akiondoka Marseille kuelekea Deportivo La Coruna, ambao ndiyo wamerejea tena katika Ligi Kuu ya Hispania, La Liga baada ya kutokuwepo kwa muda mrefu.

Kocha mpya wa timu ya taifa ya Gabon, Sebastien Migne, sasa atalazimika kufanya mipango yake bila ya kumtegemea Aubameyang wakati akiandaa timu kwa ajili ya mechi ya kwanza mwezi ujao ya kuwania kufuzu kwa AFCON ya mwakani.

Gabon wako kundi A pamoja na timu iliofika robo fainali Kombe la Dunia Morocco. Wengine kwenye kundi hilo ni Niger na Lesotho.

CHANZO:TRT Afrika Swahili