Namna Uturuki inavyosaidia Rwanda kuwafikia watalii milioni 300 kutoka eneo la Mediterania
AFRIKA
3 dk kusoma
Namna Uturuki inavyosaidia Rwanda kuwafikia watalii milioni 300 kutoka eneo la MediteraniaKukua kwa ushirikiano na Uturuki unaunganisha Rwanda, miuondombinu na uwezo wa kidiplomasia kujiweka katika nafasi nzuri ya kuimarika kwa utalii na sehemu za kufanyia makongamano.
Rwanda inajulikana zaidi na utalii wake wa Kwita Izina, sherehe ya kila mwaka ya kuwapa majina sokwe wa milimani. / Wengine .
18 Februari 2026

Wakati Rwanda ilipokuwa na Maonesho ya Kimataifa ya Mashariki mwa Mediterania ya Utalii na Usafiri (EMITT) jijini Istanbul mapema mwaka huu, nchi hiyo imekuwa ikilenga jambo mahsusi: kupata kufikia sehemu ya watalii milioni 300 ambao hupitia mashariki mwa Mediterania kila mwaka.

"Eneo la Mashariki mwa Mediterania, likichukuliwa kama sehemu moja ya kitalii, ni moja ya eneo kubwa duniani," Charles Kayonga, balozi wa Rwanda nchini Uturuki, ameiambia TRT Afrika. "Linapokea watalii milioni 300 kila mwaka kati ya milioni 900 kote ulimwenguni. Kwa Rwanda, ambayo inajiweka katika nafasi ya kuwa kitovu cha utalii, soko hili ni muhimu kimkakati."

Ndoto hiyo iko katika nguzo tatu: wanyamapori na bayoanuai, kutokana na sokwe wa milimani katika Mbuga ya Taifa; sekta ya mikutano na makongamano inayokuwa kwa kasi, na sifa ya kuwa nchi salama zaidi kwa wageni barani Afrika.

Kayonga anaeleza Rwanda kuwa "na uwezo mkubwa kitalii", akizungumzia kuhusu uwekezaji wa serikali katika sekta ya hoteli na miundombinu ya maeneo ya mikutano kwa kile anachokiita utamaduni wa kutoa huduma unaoimarika.

Yote haya hayawezi kufanya kazi bila muunganiko wa safari za ndege na miundombinu, na ndipo ambapo umuhimu wa Uturuki unahitajika kama moja ya nchi washirika wa muda mrefu.

Shirika la Ndege la Turkish Airlines lina safari kadhaa kila wiki kutoka Kigali, kuisogeza Rwanda hadi Istanbul na kuiunganisha na bara Ulaya, Asia na kote Mediterania.Kwa wafanyabiashara, wajumbe wa mikutano na watalii wanaotaka kujiburudisha, ugumu wa kuelekea katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki isiyo na bahari umeondoka.

Safari hizo za ndege zimejumuishwa katika mpango wa makubaliano karibu 30 kati ya serikali hizo mbili, huku ushirikiano katika utalii ukiwa muhimu zaidi.

"Mazingira ni mazuri na ndiyo ilivyo kwa uhusiano," anasema Kayonga.

Nchi hiyo ilikuwa mwenyeji wa mashindano ya kuendesha Baiskeli ya Dunia UCI – ikiwa ni mara ya kwanza kwa mashindano hayo ya dunia kufanyika katika ardhi ya Afrika – hivi karibuni, kutoa fursa kwa wageni kuona miundombinu yake mizuri ya barabara.

"Kuna uwezo mkubwa barani Afrika," anasema Kayonga. "Natamani tungeweza kuimarisha uwezo kupitia ushirikiano kama tulivyofanya kati ya Rwanda na Uturuki."

Ikiwa asilimia 70 ya watu wake wakiwa chini ya umri wa miaka 35, Rwanda pia imejiweka katika nafasi ya kuwa kitovu cha mikutano ya vijana, ubunifu na mashindano ya kimataifa ya michezo.

Mchango wa Uturuki unakuja kupitia ufadhili wa masomo, kuendeleza vipaji na mafunzo yanayolenga sekta ya teknolojia.

Uongozi wa Rais

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame wamekuwa wakishirikiana kupitia mikutano mbalimbali na kutembeleana na miaka kadhaa.

Kayonga anasema ni kutokana na umuhimu wa ushirikiano wa karibu kati ya viongozi hao.

"Hatuwezi kuwa na uhusiano wa karibu zaidi ila kuwa na uongozi thabiti," anasema. "Rais Kagame na Rais Erdoğan wameimarisha uhusiano wao."

Uhusiano huu umefanya kuwepo kwa mifumo ya makubaliano, ushirikiano wa kibiashara na kuimarisha uhusiano wa watu wa mataifa hayo mawili.

Kayonga ambaye mwenyewe amesafiri katika maeneo mengi nchini Uturuki. "Naipenda hii nchi sana. Ni nzuri na ina historia thabiti. Unasafiri sehemu unakutana na vito vya kihistoria na ushahidi wa utamaduni halisi," anasema.

Kwa Rwanda, uhakika wa mkakati huu uko wazi. Taifa dogo, barani Afrika ambalo halina bahari lenye ndoto kubwa linahitaji washirika ambao wanawaunganisha, kuleta uwekezaji na umuhimu wa kidiplomasia.

Uturuki, ambayo kitovu chake ni Istanbul, ujuzi wake katika ujenzi na sera yake ya faida kwa wote katika kuongeza ushawishi wake barani Afrika, ina sifa zote za mshirika mzuri. Iwapo kama watalii milioni 300 wataanza safari zao za kwenda kuona sokwe ni suala la kuangazia.

Lakini kwa sasa sehemu ya kutua, tayari, imeshaandaliwa.

CHANZO:TRT Afrika English
Soma zaidi
Afrika Kusini yaomba utulivu kufuatia maandamano dhidi ya kusimikwa kwa 'Igwe' wa Nigeria
Rwanda ‘yahofia’ operesheni za DRC dhidi ya kikundi cha FDLR
Kenya yalipa ada ya Dola milioni 30 ya uenyeji wa AFCON 2027
Hasara ya mamilioni kufuatia ubomoaji katika soko kubwa zaidi la wazi la Gikomba Nairobi
Shabiki maarufu ‘Lumumba Vea’ akosa viza ya  kwenda kuishangilia DRC dhidi ya Jamaica
Mamlaka ya uchukuzi Kenya yazindua ukaguzi wa lazima wa afya kwa madereva ili kupunguza ajali
Tanzania yahimiza matumizi ya AI kuimarisha mtangamano na maendeleo EAC
Kundi lenye silaha limewaua watu wasiopungua 20 Jimbo la Plateau nchini Nigeria
Wafungwa wasiopungua 11 wafariki kutokana na mlipuko wa kipindupindu katika jela DRC
Kagame awaamuru maafisa waandamizi wa serikali 'kusimama' wakati wa hotuba yake
Wadukuzi wadukua maombi ya kazi 450,000 nchini Afrika Kusini
Rais wa Misri asema ni Trump pekee anaweza kusimamisha vita, aonya kupanda zaidi kwa bei ya mafuta
Togo yatoa uzoefu wa kupambana na magonjwa yasiyopewa kipaumbele
Watu 15 wamefariki katika ajali ya barabarani mkoa wa kati Kenya
Mahakama kuu ya Jamhuri ya Congo imethibitisha ushindi wa Sassou Nguesso kwa awamu ya tano
Rwanda, Burundi wanagombana juu ya juhudi za rais wa zamani wa Senegal Sall kuongoza UN
Vifo kutokana na mafuriko nchini Kenya vyaongezeka hadi 108, polisi wasema
Majenerali wakuu wa Uganda wazuiliwa kwa madai ya ufisadi: ripoti
Eswatini yamrudisha nyumbani mwananchi wa Cambodia aliyefukuzwa kutoka Marekani
Waasi waanza kuondoka katika vijiji vya DRC ili kuhimiza amani