Kesi ya uhalifu inayomkabili Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu imeahirishwa kutokana na sababu za kiusalama, kulingana na jarida la The Jerusalem Post.
Majaji wa mahakama ya wilaya ya Yerusalemu siku ya Jumapili, waliamua kusikiliza ushahidi kutoka kwa shahidi mwingine, na hivyo kuchelewesha zamu ya Netanyahu kupanda kizimbani kutoa ushahidi wake.
Uamuzi huo, unafuatia ombi kutoka upande wa utetezi wa kusitisha ushahidi wa wa Netanyahu, ikitoa sababu za kiusalama.
Hata hivyo, upande wa waendesha mashitaka walipinga ombi hilo, wakisisitiza uwepo wa hoja ya msingi ya kiusalama na kumtaka Netanyahu afuate kalenda ya mahakama hiyo kwa maslahi ya umma.
Kesi hiyo ipo katika hatua ya mahojiano na Netanyahu, ambapo kwa mara ya kwanza, waziri mkuu huyo alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Disemba 2024.
Netanyahu anashtakiwa kwa makosa ya ufisadi na udanganyifu, iliyofunguliwa Novemba 2019.
Mbali na kesi hiyo, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilitoa hati ya kukamatwa kwa mwanasiasa huyo Novemba 2024, kwa makosa ya uhalifu wa kibinadamu unaoendelea huko Gaza.















