| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Uturuki, Saudi Arabia wafanya mazungumzo ya ngazi ya juu Ankara, wajadili uhusiano, masuala ya kanda
Awali, mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa yote mawili waliongoza kikao kwa pamoja cha mkutano wa tatu wa Baraza la Uratibu la Uturuki na Saudia Arabia.
Uturuki, Saudi Arabia wafanya mazungumzo ya ngazi ya juu Ankara, wajadili uhusiano, masuala ya kanda
Rais wa Uturuki amemkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia mji mkuu Ankara. / AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Faisal bin Farhan Al Saud katika mji mkuu Ankara.

Mkutano huo wa faragha katika Ikulu ya Rais siku ya Jumatano pia ulihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje Hakan Fidan, Mkuu wa Mawasiliano Burhanettin Duran, Msaidizi Mkuu wa Rais Hasan Dogan, na mshauri mwandamizi wa sera ya mambo ya nje Akif Cagatay Kilic.

Awali, mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zote mbili waliongoza kikao kwa pamoja cha mkutano wa tatu wa Baraza la Uratibu la Uturuki na Saudia Arabia, wakijadili uhusiano wa mataifa yote mawili na yanayojiri katika kanda, ikiwemo Gaza.

Katika taarifa kwenye mtadano wa kijamii wa NSosyal, Fidan amesema mkutano huo ulifanyika huku wizara husika na taasisi za nchi zote mbili zikishiriki.

Kuimarisha uhusiano wa mataifa mawili

Alisema pande zote zilitathmini kazi za kamati katika maeneo ya kimkakati kama biashara, nishati, ulinzi, elimu, utamaduni, utalii, na uchukuzi, huku wakiangazia uhusiano wa mataifa hayo mawili kitaasisi.

Fidan pia alisema mazungumzo yaliangazia masuala ya kikanda, hasa hali ya Gaza, na nchi zote mbili zikatia saini makubaliano kuondoa viza kwa wenye hati za kusafiria za kidiplomasia na zile maalum.

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki alimshkuru mwenzake wa Saudi Arabia na ujumbe wake kwa ziara yao, akieleza matumaini kuwa makubaliano yaliyofikiwa yatakuwa na faida kwa mataifa yote mawili.

CHANZO:AA