Dkt. Kabir Adamu
Eneo la kati la Sahel linapitia mabadiliko makubwa katika kanda kufuatia kujiondoa kwa Burkina Faso, Niger na Mali katika ECOWAS na kuanzisha Muungano wa Mataifa ya Sahel (AES).
Kile kilichoanza kama mapinduzi ya kijeshi nchini Mali, Burkina Faso na Niger kimekuwa ushirikiano wa kiusalama, uhusiano wa kitaasisi na ushawishi ulioenea hadi kwa nchi jirani kama vile Algeria na Morocco na kusababisha ushindani wa uwezo.
AES, kwa sasa imejitambulisha kisiasa na kiulinzi nje ya ECOWAS.
Agosti 9, 2026, Algeria iliwapa Niger helikopta mbili za kushambulia za Mi-24V na helikopta mbili za wanajeshi za Mi-171, pamoja na silaha, na vipuri.
Kutolewa kwa helikopta hizo, kulikoamriwa na Rais Abdelmadjid Tebboune, kulielezwa kuwa ni kuimarisha uhusiano na kuchangia usalama katika kanda. Hii iliashiria upatanishi wa kijeshi kati ya Algeria na AES baada ya kutofautiana kufuatia kuangushwa kwa droni ya Mali karibu na mpaka wao Aprili 2025.
Tukio hilo lilisababisha mabalozi kuondolewa katika nchi tatu za mataifa ya AES na marufuku ya kutumia anga za nchi hizo. Kuanzia mapema 2026 Algeria ilibadilisha hilo kwa kutumia diplomasia ya nishati na miundombinu, kuzungumza na uongozi wa Niger, na kuanzisha tena mifumo ya ulinzi mpakani.
Kutolewa kwa helikopta hizi kulikamilisha muendelezo wa msaada wa kijeshi kwa mataifa ya AES kutoka kwa Algeria.
Kutafuta ushawishi Afrika Magharibi
Wakati huohuo, tofauti za Algeria na Morocco katika Sahel kuna hatari ya kusababisha mkawaruzano zaidi wa kisiasa kwenye hali ambayo iko tete, hata wakati mataifa ya AES yakijaribu kufaidika na ushindani huo.
Nigeria iko katika hali ngumu zaidi. Wote wanakabiliwa na hatari ya usalama katika mpaka wa Niger na katika Ziwa Chad inafanya Nigeria kushirikiana na Niger.
Ushawishi unaongezeka kupimwa kwa uwezo wa ushirikiano na wengine.
Iwapo kama ushirikiano utaimarisha usalama au kama itakuwa ushirikiano tu bila tija itategemea na hali ya kubadilishana taarifa za intelijensia, kuimarisha uhusiano wa mataifa mawili, na utashi wa kila upande kupunguza hatari.
Ramani ya Sahel inachorwa tena upya kwa ushirikiano kati ya mataifa, taasisi kugawanywa na kutafuta ushawishi. Matokeo yake yataonekana zaidi ya miji mikuu mitatu ya mataifa ya AES, kutoa muelekeo kwa mfumo kamili wa usalama Afrika Magharibi kwa muongo mzima ujao.
Mwandishi, Dkt. Kabir Adamu, ni Mkurugenzi Mkuu, Shirika la Beacon Security and Innovations Limited, shirika la masuala ya usalama lenye makao yake jijini Abuja.
Kanusho: Maoni ya mwandishi hayaakisi maoni, mitazamo na sera ya uhariri ya TRT Afrika.























