| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Marekani yalaumiwa kwa kusema Ethiopia 'ni ya pili kwa uchumi mkubwa Afrika'
Watumiaji wa mitandao ya kijamii wanasema kosa hilo linaonesha kuwa maafisa wa Marekani hawana ufahamu wa kutosha kuhusu bara hilo.
Marekani yalaumiwa kwa kusema Ethiopia 'ni ya pili kwa uchumi mkubwa Afrika'
Balozi wa Marekani Ervin J. Massinga wakati wa Kongamano kati ya Sekta ya Umma na Binafsi jijini Addis Ababa.

Marekani inalaumiwa kwa kusema kimakosa kuwa Ethiopia "ni ya pili kwa uchumi mkubwa barani Afrika" huku akipongeza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili chini ya serikali ya Trump na sera yake ya mambo ya nje ya "Marekani Kwanza".

Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema katika mtandao wa kijamii Jumatatu, Agosti 24, kuwa ''ushirikiano huu utafanya Marekani iwekeze na kupatikana tija zaidi kwa Wamarekani na Waethiopia kutoka nchi yenye uchumi wa pili kwa ukubwa barani Afrika."

Watumiaji wa mitandao ya kijamii waliilaumu kwa kusema Ethiopia ni ya pili kwa uchumi mkubwa barani, huku wengine wakisema kuwa taarifa hiyo ni ya kupotosha, na wengine wakisema kuwa maafisa wa Marekani hawana ufahamu wa kutosha kuhusu bara la Afrika.

Ethiopia ni ya tisa kwa uchumi mkubwa barani Afrika, kulingana na takwimu za Shirika la Fedha Duniani (IMF). Mataifa matatu yenye uchumi mkubwa duniani ni Afrika Kusini, Misri na Nigeria.

Makosa haya ya sasa hivi yanakuja wiki kadhaa baada ya Marekani kuchakachua ramani ya Afrika, ikionesha mipaka tofauti ya nchi mbalimbali wakati wa mkutano wa kimataifa nchini Brazil, jambo lilowaghadhabisha wengi.

CHANZO:TRT Afrika English
Soma zaidi
Jenerali wa DR Congo miongoni mwa watu 13 waliofariki katika ajali ya ndege
Afrika itapata hadhi ya uwanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa?
Sudan yashtumu taarifa za Marekani zinazohoji uhalali wa serikali huku viza ya Burhan ikizua utata
Mke wa Besigye awataka viongozi wa Afrika wazungumzie masuala ya haki za binadamu
Waasi wa Tigray 'wadhibiti' uwanja wa ndege wa kanda ya Ethiopia
Tanzania yatoa wito wa amani Gaza
Sudan yaahidi kukabiliana na mfumuko wa bei huku vita vikiathiri uchumi
Makundi saba yenye silaha yaunda muungano nchini Ethiopia
Afrika Kusini yawakamata washukiwa watatu baada ya miili tisa wanawake kupatikana
9 wauawa kwa kupigwa risasi katika Jimbo la Plateau nchini Nigeria
Jeshi la Namibia lakumbwa na shambulio la mtandaoni
Simba kumi wakutwa wamekufa katika hifadhi ya Ngorongoro nchini Tanzania
Kuanzia watoto watano hadi mapambano ya kuishi: Changamoto ya uzazi wa watoto wengi barani Afrika
Jeshi la Sudan lawaua wapiganaji wa RSF na kuharibu magari tisa katika eneo la Blue Nile
Mswada mpya Sudan Kusini kumpa Salva Kiir mamlaka yote ya kuwafuta kazi Makamu wake kabla uchaguzi
Sudan Kusini inasonga mbele na mipango ya mradi wa Bwawa la Grand Fula kwenye mto White Nile
Marekani inatuma dola milioni 2.5 nchini Gambia kutokana na mauzo ya kasri la rais wa zamani
Afrika Kusini yatoa zawadi ya $24,600 kwa taarifa kuhusu muuaji wa wanawake
TikTok kukata kodi kwenye mapato ya waandaaji maudhui Kenya
Mkuu wa polisi Kenya apatikana na hatia ya kudharau mahakama kufuatia maandamano ya Gen Z