Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini Tanzania (EWURA) imetangaza bei mpya za nishati ya mafuta zinazoanza kutumika Mei 6, 2026.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo, nishati ya petroli imeongezeka kutoka Dola 1.47 (Shilingi 3,820) hadi Dola 1.59 (Shilingi 4,115) kwa lita.
Wakati huo huo, lita moja ya dizeli, sasa itapatikana kwa Dola 1.67 (Shilingi 4,248) kutoka Dola 1.47 (Shilingi 3,806) kwa lita, kwa mkoa wa Dar es Salaam.
Kulingana na EWURA, mabadiliko ya bei hayo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na vita inayoendelea eneo la Mashariki ya Kati, ikihusisha Marekani, Israel na Iran, pamoja na kufungwa kwa Mlango Bahari wa Hormuz unaopitisha takriban asilimia 20 ya mafuta yote yanayosafirishwa duniani.
Maeneo ambayo yatashuhudia gharama kubwa za mafuta ni pamoja na mikoa ya Mwanza, Geita, Kagera na Katavi ambapo nishati hiyo itapatikana kwa Dola Duniani kumeathiri upatikanaji na gharama za mafuta katika soko la kimataifa.
Baadhi ya mikoa ambayo bei ya petroli ipo juu zaidi ni Mwanza, Kigoma, Geita, Kagera na Katavi ambapo itapatikana kwa gharama ya Dola 1.66 (Shilingi 4,300).


















