tokea masaa 2
Rais wa Marekani Donald Trump alielezea muungano huo kama “dhaifu japo unaonekana kuwa na nguvu” (paper tiger), na alisema kuiondoa Marekani kutoka katika mkataba huo wa ulinzi sasa “hakuhitaji tena kufikiria upya,” kulingana na mahojiano na gazeti la Uingereza, Daily Telegraph. Alisema kwa muda mrefu amekuwa na mashaka kuhusu uaminifu wa NATO.
“Ndiyo kabisa, ningesema [jambo hilo] halihitaji tena kufikiria upya,” Trump aliliambia gazeti hilo alipoulizwa kama angeweza kubadili uamuzi kuhusu uanachama wa Marekani katika muungano huo baada ya mgogoro.
“Sikuwahi kushawishika na NATO. Siku zote nilijua walikuwa dhaifu japo wanaonekana kuwa na nguvu, na Putin anajua hilo pia, kwa kweli.”
CHANZO:Reuters










