Namna kijana mwenye umri wa miaka 12 mwenye usonji alivyotumia uokaji keki kukabiliana na chuki
ULIMWENGU
6 dk kusoma
Namna kijana mwenye umri wa miaka 12 mwenye usonji alivyotumia uokaji keki kukabiliana na chukiBaada ya shambulizi katika msikiti mmoja Uingereza, Joshua Harris alitumia mapenzi yake ya kuoka kuwa kampeni aliyoipa jina la ‘Cake Not Hate’, harakati za kukabiliana na chuki dhidi ya Waislamu kwa kuonesha huruma.
Dan anamtambua Joshua kama ‘’balozi wa amani’’ kwa sababu anakutana na watu bila ya kuwa na unyanyapaa kama walionao watu wazima.

Kuanzia Jumatatu hadi Alhamisi, Joshua Harris anafanya shughuli ya kuoka.

Iikifika Ijumaa kila wiki, mtoto huyo mwenye umri wa miaka 12 huulizia mkoba wake – akionesha herufi zilizochorwa kwenye mkono wa baba yake.  Neno linalofuata ni “teksi.”

Anajua ni wakati wa kuondoka.

Mwishoni mwa juma kwa Joshua huwa ni kupeleka keki ambazo amekuwa akizioka wiki nzima katika miskiti na maeneo mengine ya ibada kote nchini Uingereza.

Kwa Joshua, anayejulikana mitandaoni “Joshie Man”, kuoka kwake ni jambo analolipenda kabla hata ya kuwa maarufu. Mama yake, Herica Harris, alimfundisha kuoka.

“Mke wangu, Herica, ana umri wa miaka 48 na ni mke nyumbani. Ametumia muda wake mwingi kuwalea watoto wetu, Joshua na dada yake mwenye umri wa miaka 10, Charlotte,” anasema baba yake, Dan Harris, mwenye umri wa miaka 47.

Dan anasema Joshua amepika katika mikahawa kadhaa yenye hadhi ya nyota ya Michelin, kutembelea majiko ya Ritz London na kukutana na wapishi maarufu wa Uingereza, ikiwemo Jamie Oliver na Tommy Banks.

Lakini baada ya shambulizi la watu wa mrengo wa kulia katika msikiti kwenye mji wao wa Peterborough, keki ikawa zaidi ya jambo ambalo Joshua analipenda. 

“Alikuwa anapenda sana kupika, alafu ikatokea kuwa keki ndiyo yake ya kuwasilisha ujumbe,” Dan ameiambia TRT World.

Kampeni ya ‘Cake Not Hate’

Joshua ni mvulana mwenye usonji ambaye hazungumzi na anaishi na familia yake mjini Peterborough. Kampeni ya ‘Cake Not Hate’ ilianza baada ya wanaharakati wa mrengo wa kulia kuingia katika msikiti, kumshambulia polisi wa kike na kuwatusi watoto na waumini wengine, kulingana na Dan.

Kutokana na tukio hilo, baba na mtoto wakaenda kwenye msikiti huo siku ya pili wakiwa wamebeba keki. 

Dan, Muingereza ambaye ni Mkristo mzungu, alitaka Waislamu wafahamu kuwa wale wanaendeleza chuki dhidi ya Waislamu hawawakilishi Uingereza yote.

“Lengo ilikuwa kufanya hivyo mara moja kipindi cha mvua siku ya Jumapili mchana.” Badala yake, video ya ziara yao ikasambaa zaidi ya mji wa Peterborough.

Wawili wakaanza kwenda katika miskiti zaidi kote Uingereza.

Pia wamefikisha ujumbe wao katika makanisa, masinagogi, mahekalu, kuashiria azma ya Dan kuwa mshikamano ni zaidi ya mipaka ya dini kuliko kuweka mipaka mingine.

Harakati zao siyo kujibu ishara ya chuki kwa kugombana. Wanatumia ukarimu: keki ya kuokwa nyumbani, mazungumzo na maamuzi ya kufika maeneo ambayo wengine wametiwa hofu kufikia.

Dan anamueleza mtoto wake kama “balozi wa amani”, siyo kwa sababu Joshua hutoa hotuba au kushiriki mijadala ya kisiasa, lakini kwa sababu mtazamo wake kwa watu si wa kunyanyapaa na mara nyingi yanatoa muelekeo kwa watu wazima. 

“Hajali kuhusu rangi ya ngozi yako, imani yako au asili yako. Anafahamu kama mtu ni mkarimu au siyo mkarimu,” Dan anasema. 

Dan alijichora tattoo ya herufi zote alipotambua kuwa mtoto wake anahitaji sehemu ya kuwasiliana — ile ambayo ingemsaidia pale ambapo hana sehemu ya kutumia kompyuta na anahitaji mawasiliano ya haraka.

Ukarimu ulikabiliwa na vitisho

Wakati harakati hizo zikiendelea, pia kulizuka uhasama kutoka kwa wafuasi wa siasa za mrengo wa kulia. Dan anasema wengine walichukulia kuunga kwake mkono Waislamu kama kusaliti Uingereza, licha ya kuwa alifahamu kuwa sehemu ya maadili ya nchi yake.

Anasema Stephen Yaxley-Lennon, maarufu Tommy Robinson, aliandika ujumbe kuhusu familia hiyo na kuweka picha ya Joshua kwenye mtandao wa X. Dan anasema vitisho vimezidi baada ya familia hiyo kuanikwa zaidi kwenye mitandao.

Familia hiyo imekabiliwa na vitisho vya vifo na vurugu. Watu walijaribu kufahamu sehemu ambayo Dan anafanya kazi na shule ya Joshua, huku barua ikisambazwa miongoni mwa watu wanaoamiliana nayo Dan wakiwataka wakae mbali naye na kumtaja kuwa hatari na ‘siyo Muingereza’.

Vitisho hivyo vilifanya baba na mtoto kubadilisha namna wanavyofanya safari zao. Sasa polisi nchini Uingereza huongozana nao wanapokwenda miskitini, wakati mwingine wakiwasubiri nje na kuwasindikiza wanapoingia ndani ya majengo.

Dan anasema polisi wamewasimamia haki zao za kujieleza hadharani na sehemu za ibada, hata wakati vitisho hivyo vinapofanya hali kuwa mbaya.

Kwa Dan, kuacha kufanya wanachofanya itakuwa ni kuruhusu vitisho badala ya kuendelea na mshikamano. 

“Kama nitakubali kutishwa na fursa yote niliyonayo katika maisha yangu, itakuwaje kwa watu wengine?” anasema.

Kwa nini miskiti ni muhimu  

Kuonekana na watu kunaweza kuwa na uzito kwa Joshua. 

Taa za zenye kung’aa, sauti kubwa, maeneo ngeni na sehemu yenye watu wengi yanaweza kumtatiza, na Dan anaeleza kuwa kufadhaika hakumaanishi kuwa ni kukosa nidhamu au heshima.

“Wakati anapokuwa na changamoto, siyo eti ni mtovu wa nidhamu,” Dan anasema. “Anapokuwa na mfadhaiko, siyo kuwa anakosa nidhamu. Huwa analemewa na mambo mengi tu.” Inajumuisha, kwa mfano, mtazamo wa mienendo kupitia kuelewa kuliko kuhukumu.

Pamoja na yote Dan anasema mara nyingi Joshua anaonekana mwenye amani anapokuwa miskitini. Kuswali kimya kimya, maeneo ya wazi ya ibada na ukarimu wa waumini huwa kunampa utulivu sana.

Jambo ambalo hatoshau ni wakati wa ziara yake mjini Medina, ambapo mamlaka za Saudi Arabia zilimualika atembelee Al Masjid an Nabawi, msikiti wa Mtume, amapo ndiyo kuna kaburi la Mtume Muhammad, rehema na amani zimfikie yeye.

Kwa Muingereza Mkristo na mtoto wake wa kiume mwenye usonji, mualiko huo ulikuwa na maana zaidi baada ya chuki walizopata wakiwa nyumbani .

“Medina unaleta hisia zaidi kuliko kuwa sehemu,” Dan anasema, akikumbuka amani, utulivu na hali ya utofauti. Familia zilikuwa bado zinatembea barabarani saa tisa usiku, na walioneshwa sehemu moja ya msikiti ambayo kwa kawaida watu wengine hawapati nafasi ya kuiona. “Sikuwa nafahamu kuna sehemu nzuri kama hiyo duniani,” aliongeza.

Siku kumi nchini Uturuki

Safari hiyo iliendelea hadi nchini Uturuki. Kati ya Julai 17 na 27, Joshua na Dan walikuwa na ziara ya siku kumi jijini Istanbul, wakitembelea miskiti kadhaa na kueneza ujumbe wao wa ‘Cake Not Hate’ na waumini pamoja na jamii za maeneo mbalimbali.

Ziara hiyo ilijumuisha maeneo ya kihistoria ya ibada, kutoka Msikiti wa Suleymaniye hadi Msikiti wa Aziz Mahmud Hudayi.

“Chini ya kipindi cha saa 48 baada ya kuwasili, Joshua aliona Mlangobahari wa Istanbul wa bluu na mara moja alitaka kuingia aogelee.”

Dan anasema mapokezi waliopata yalionesha hali tofauti ya namna Waislamu wanavyoangaziwa na baadhi ya vyombo vya habari vya Magharibi. 

Badala ya kuona watu wakiwanyanyapaa, aliona waumini wakimpa nafasi Joshua, wakimoa maji au chakula kumsikiliza kwa makini wakati anapohitaji muda peke yake.

Tarehe 22 Julai, Rais Recep Tayyip Erdogan alimlaki Joshua katika Ikulu ya Dolmabahce jijini Istanbul. Mualiko huo uliwafikia siku sita baada ya baba na mtoto kuwasili katika jiji hilo, na Dan anasema hawakuwahi kuamini kuwa kutembelea kwao miskiti kungefanya waalikwe na Rais.

Alieleza mkutano huo kuwa mzuri na anasema mara moja Erdogan alitokea kuelewana na Joshua. Rais aliikaribisha familia hiyo na kumpa Joshua zawadi mbalimbali, ikiwemo gari la kuendeshwa kwa ‘remote’ ambalo mara moja lilimfurahisha Joshua.

Mkutano huo pia ulifanya umma kuangazia suala la namna watoto wenye usonji wanawasiliana. Joshua anatumia iPad ambayo ina mfumo wa mawasiliano, ambao familia yake unauita ‘kisemeshi’ chake. 

Kwa kutumia maumbo na maneno, ina nafasi ya kujieleza, mahitaji yake na hisia bila kuzungumza.

Njia zake za kipekee za mawasiliano, kumbukumbu nzuri na mapenzi yake ya kuoka yamemuwezesha kuendeleza maisha bila kuwa mwanaharakati kama inavyofahamika na jamii kwa ujumla.

“Nisingependa kumbadilisha Joshy kwa ajili ya dunia,” Dan anasema. “Nataka kubadilisha dunia kwa ajili ya Joshy.”

CHANZO:TRT World