Nchini Ghana bado kuna athari za kale.
Karibu na jiji la Kumasi, majengo ya kitamaduni ni ishara ya mwisho ya zama za ustaarabu wa jamii ya Asante, ambao ulifikia kilele chake katika karne ya 18.
Majengo hayo yanajumuisha madhabahu kumi.
Yakiwa yamepangwa kuzunguka ua, majengo hayo yamejengwa kwa mbao, mianzi na udongo, hapo awali yalikuwa na paa za nyasi.
Kuta za kipekee za mapambo zinaonesha aina nyingi za sanaa na ubunifu.
Zina miundo na michoro ya wanyama, ndege na mimea, wanaohusishwa na ishara za jadi za "Adinkra".
Kama ilivyo kwa aina nyingine za sanaa za jamii ya Asante, miundo hii si ya mapambo tu, pia ina maana za ishara, zinazohusiana na fikra na imani za watu wa jamii ya Asante, na zimerithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Majengo hayo, rangi yao nzuri, na ustadi na utofauti wa mapambo yao ni ishara ya mwisho iliyosalia ya athari muhimu za usanifu wa kitamaduni ambao ulitoa kielelezo cha Ufalme wa Asante uliokuwa na na ushawishi mkubwa, uwezo na utajiri wa mwishoni mwa karne ya 18 hadi mwishoni mwa karne ya 19.
Majengo ya asili ya Asante yanaakisi na kuimarisha urithi tata kiustadi, kidini na kiimani.
Imani za jadi, ambazo bado zinafuatwa katika madhabahu ya Asante, zinahusisha kuwasiliana na miungu kutafuta ushauri kuhusu hali mahsusi, au kabla ya kutekeleza jambo muhimu.
Ndio maana madhabahu yamedumishwa yakiwa kamala yalivyo na umuhimu wake wote.
Hata hivyo, huku tukiwa katika zama tofautim, majengo haya muhimu ya kitamaduni yanaharibika . Kwa kuwa yametengenezwa kwa udongo na majani, yako kwenye hatari ya kuathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa.











