| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Uganda bado iko katika hatari kutokana na mlipuko wa Ebola DRC: WHO
Uganda bado iko kwenye hatari kutokana na mlipuko wa ugonjwa katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema siku ya Jumatano.
Uganda bado iko katika hatari kutokana na mlipuko wa Ebola DRC: WHO
Mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ulitangazwa katika taifa lililo jirani na Uganda, la DRC, katikati ya mwezi Mei 2026.

Uganda bado iko katika hatari kutokana na mlipuko wa Ebola katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, WHO ilisema siku ya Jumatano baada ya nchi hiyo kufurahia kumalizika kwa maambukizi ya ugonjwa huo katika taifa hilo.

Uganda ilikamilisha siku 42 tangu mgonjwa wa mwisho aliyekuwa ameambukizwa kuruhusiwa kutoka hospitali Juni 16, na tangu wakati huo hakujakuwa na maambukizi yoyote yaliyothibitishwa.

Siku ya Jumanne, wizara ya afya ilisema "imefarijika kutangaza rasmi kuwa Uganda haina tena maambukizi ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola 2026", ikiongeza: "Sasa hivi, hakuna tena Ebola Uganda."

Lakini Shirika la Afya Duniani limesema utaratibu wa kimataifa ni kuwa siku 42 baada ya kufanya tathmini ya mtu wa mwisho aliyetangamana na mgonjwa aliyekuwa ameambukizwa.

Maambukizi zaidi ya 3,000 ya Ebola DRC

Siku arobaini na mbili ni muda mrefu wa kutathmini kama maambukizi ya Ebola yapo au hayapo.

"Kwa kuwa mgonjwa wa mwisho aliyeambukizwa na ugonjwa huo ulioanzia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo aliruhusiwa kutoka hospitali Julai 16, kwa hiyo WHO itaanza kufanya tathmini yake kwa siku 42 kuanzia siku hiyo ili kujihakikishia kuwa hakuna msururu wa maambukizi," shirika hilo la Umoja wa Mataifa lilisema.

Kumekuwa na maambukizi 3,360 yaliyothibitishwa, ikiwemo vifo 1,487 nchini DRC, mlipuko ukiwa zaidi katika mkoa wa kaskazini mashariki wa Ituri.

Uganda, ambayo mpaka wake uko karibu na Ituri, imekuwa na maambukizi 20 yaliyothibitishwa, ikiwemo vifo viwili vilivyothibitishwa, na sasa wagonjwa 18 waliopona.

CHANZO:TRT Afrika Swahili