| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Mwanasiasa wa upinzani Uganda Besigye alazwa ICU baada ya kuanguka mahakamani: mke wake
Kizza Besigye, ambaye alianguka wakati akiwa mahakamani Jumatano, amelazwa ICU katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Mulago, kama alivyosema mkewe.
Mwanasiasa wa upinzani Uganda Besigye alazwa ICU baada ya kuanguka mahakamani: mke wake
Mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye, akiingizwa kwenye gari la wagonjwa baada ya kuzimia alipokuwa mahakamani Kampala, Julai 29, 2026.

Mwanasiasa maarufu wa upinzani nchini Uganda, anayekabiliwa na mashtaka ya uhaini, amelazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Mulago nchini Uganda, kwa mujibu wa mke wake Winnie Byanyima ambae ameandikia katika mtandao wa X mapema Alhamisi.

Besigye mwenye umri wa miaka 70, alianguka akiwa mahakamani jijini Kampala Julai 29, 2026 na kukimbizwa hospitali kwa kutumia gari ya wagonjwa kwa ajili ya matibabu.

Winnie Byanyima, ambae pia ni mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UNAIDS, amesema mume wake amelazwa katika Hospitali ya Mulago.

"Hana fahamu, hawezi kuongea, na pia hajazinduka licha ya dawa za maumivu," amesema.

Msemaji wa serikali Alan Kasujja hakupokea simu ya Reuters pindi alipotakiwa kuliongelea suala hilo.

Besigye amekuwa kuzuizini tangu Novemba 2024 baada ya kukamatwa akiwa na msaidizi wake Obeid Lutale na kushtakiwa kwa uhaini.