| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Erdogan wa Uturuki, Faye wa Senegal wajadili uhusiano, masuala ya dunia
Uturuki itaendeleza juhudi za mpango wa "faida kwa wote" na Senegal, Rais Recep Tayyip Erdogan amesema.
Erdogan wa Uturuki, Faye wa Senegal wajadili uhusiano, masuala ya dunia
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye jijini Ankara, Oktoba 31, 2024.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye siku ya Jumatatu walijadili uhusiano wa mataifa yao mawili pamoja na masuala ya kikanda na dunia, mawasiliano yao yakifanyika kwa njia ya simu, kwa mujibu wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki.

Rais Erdogan anasema Uturuki itaendeleza juhudi za kuhakikisha mataifa hayo mawili yanafikia malengo ya kiwango cha biashara kati yao.

Anasema kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali, hasa uwekezaji, kutachangia zaidi katika mchakato huo.

Rais wa Uturuki pia alisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano katika sekta ya ulinzi, akisema Uturuki itaendeleza misingi ya mtazamo wa "faida kwa wote".

CHANZO:Anadolu Agency